Mchipuko

Jinsi ya kulipia wasafi Tv ukiwa na king’amuzi Cha startimes ama Azam Tv

Jinsi ya kulipia wasafi Tv ukiwa na king’amuzi Cha startimes ama Azam Tv

Jinsi ya kulipia wasafi Tv startimes

Jinsi ya kulipia wasafi Tv startimes

Kwa wale wote wenye king’amuzi Cha startimes, ni habari njema kwenu maana kwa sasa munaweza kuitazama wasafi Tv. Kampuni ya star media ilitangaza hivi majuzi kwamba imeongeza chaneli ya wasafi Tv kwenye orodha ya chaneli zinazopeperushwa na startimes.

Chaneli ya wasafi ilianza kuonekana kwenye king’amuzi Cha startimes tarehe kumi na nane na iliziduliwa katika hoteli ya slipway iliyoko masaki jijini dar es salaam.

Kulingana na utafiti wetu, startimes ni king’amuzi kinachotumika zaidi nchini tanzania na huenda kikawapa nafasi zaidi, watazamaji wa wasafi Tv na kuifanya wasafi Tv kuwa maaruufu zaidi.

Kupata wasafi Tv sio lazima uwe na hela nyingi na unaweza pata chaneli hii kwenye vifurushi tofauti kama ‘NYOTA’ kwa shilingi 7,000 kwa mwezi mmoja, kifurushi Cha ‘MAMBO’ kwa Bei ya Elfu kumi na tatu kwa mwezi na ‘UHURU’ kwa Bei ya 24,000 tu.

Jinsi ya kulipia wasafi Tv kwenye king’amuzi Cha Azam.

Jinsi ya kulipia wasafi Tv kwenye king'amuzi Cha Azam.

Je wajua kwa shilingi Elfu moja peke yake unaweza ukapata burudani kwa mda wa mwezi mmoja? Hii Ina maana sio lazima uwe na pesa nyingi kupata wasafi Tv kwenye king’amuzi Cha Azam.

Ili kupata hii burudani, hakikisha uko na kifurushi chochote cha king’amuzi Cha Azam Tv alafu fanya malipo ya 1,000 kupitia mitandao ya simu kama kawaida. Kwa kulipia wasafi Tv, chukua simu yako ya mkono na ubonyeza kama ifuatayo,

1. Piga *150*50*5# baada ya malipo kukamilika.

2. 2. Chagua lugha

3. 3. Chagua namba 3. Sajili Huduma Mpya

4. 4. Ingiza namba yako ya kadi Chagua namba 5. Wasafi TV Add On

5. 5. Utapata ujumbe wa SMS kuthibitisha usajili.

Baada ya kukamilisha haya yote utapata burudani ya Hali ya juu ndani ya wasafi kwa mwezi mzima bila kukatiziwa na yeyote.

Soma hii pia ( jinsi ya kulipia king’amuzi Cha Azam)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *