MchipukoSanaa

Utajiri wa diamond platnumz 2021

Utajiri wa diamond platnumz 2021  wawashangaza wengi kwani msanii huyu anazidi kufanikiwa kila kuchao. Wengi walifikiria labda baada ya miaka kadhaa msanii huyu angeshuka kimziki na Kipesha ila sivyo kabisa kwani hela inazidi kuingia.

Wasafi tower

Bali na nyumba ya diamond platnumz kuwa ya kifahari, inasemekana amemaliza mjengo inayojulikana kama wasafi towers. Mjengo huu upo jijini dar na inasemekana umemgharimu mabilioni ya pesa

nyumba ya diamond platnumz inajulikana kama wasafi rowers

Diamond ni mmoja wa wasanii tajiri afrika na anazidi kuingia hela zaidi kadri anavyoendelea kuachia nyimbo mpya. Haya maneno aliyasema pia mwenyewe katika radio ya wasafi anayoimiliki.

Msanii huyu ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo yake mpya Waah! Kwa sasa anamiliki vitu vingi vya dhamani zikiwemo magari ya kifahari na nyumba zinasemekana kugharimu pesa nyingi. Kusema kweli kwa sasa benki yake inampa uso wa tabasamu kila anapotazama bakio.

Utajiri wa diamond platnumz 2021

Diamond platnumz anaingiza hela nyingi kutoka mitandaoni Kama vile itunes na youtube. Hapendi maigizo kuhusu utajiri wake na unaposikia akisema mwenyewe kuwa kwa sasa ana hela nyingi ujue ni ukweli na hafanyi kama wasanii wengine wanavyofanya kutangaza kuwa Wana hela na hawana kitu kwa benki.

Wengi labda hufikiria kuwa hela nyingi diamond platnumz huzipata kwa youtube ila sivyo. Akiongea ndani ya wasafi Fm, diamond alieleza kwenye pesa yake ya mziki hutoka. Hii haimanishi kuwa msanii huyu hapati pesa kwa youtube, kumbuka ana zaidi ya watazamaji 4 billions kwenye account yake ya youtube.

” Naelewa kuwa kuna njia nyingi za kupata pesa kwenye mitandao na kwa sasa mziki wangu unapatikana kwa platform karibia zote. Platform inayonilipa zaidi ni apple music,” alisema diamond platnumz.

Najua wengi walifikiria diamond platnumz hupata pesa zake kwa tamasha pekee ila kwa leo mshajua msanii huyu anauza mziki zaidi ya msanii mwingine barani afrika. Hata kama Kuna janga la covid-19, msanii huyu anaendelea kuachia nyimbo baada ya nyingine huku Waah aliyoshirikisha koffi Olomide ikizidi kupepea ulimwengu mzima. Diamond platnumz huchukulia mziki wake kama biashara na kusema kweli anaijulia.

Diamond platnumz alipeana mfano hai na kuyasema haya ; ” wakati ninapopata views milioni kwa youtube, napokea laki sita za tanzania ila kwa itunes nikipata download milioni, hupata 2.5b pesa za tanzania”

Kwa msanii huyu kupata download milioni moja kwa mwezi ni kitu rahisi maana jina lake lipo juu na ni mmoja wa wasanii wanaosikizwa sana barani afrika.

“Ningependa kuwaomba mafans wangu wazidi ku download mziki wangu ndani ya itunes na sio mziki wangu tu pia mziki wa wasanii wengine ili tuweze kuwajenga kimaisha…. Hii njia ndio inamuezesha msanii kama drake kununua ndege za kibinafsi” … Alisema diamond

Kwa sasa Litawachoma, nyimbo aliyoshirikisha Zuchu na Waah aliyoshirikisha koffi Olomide zinapata utazamaji mkubwa sana ndani ya youtube na pia radio na Tv barani afrika zinazidi kupeperusha hizo nyimbo.

Soma hii pia ( wasanii matajiri tanzania)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *