MaishaMchipuko

Mose Iyobo aeleza sababu ya kuachana na Aunty Ezekiel

Mose Iyobo aeleza sababu ya kuachana na Aunty Ezekiel; Kwa mda sasa Aunty Ezekiel na Musa Iyobo wamekuwa hawapo pamoja na Kulingana na taarifa za hapa na pale, Musa Iyobo ako na mpenzi mpya anayesemekana kuwa ni Ruby.

Wawili hawa walikutana katika tamasha ya MTV base. Huko walikuwa timu nzima ya diamond platnumz. Aunty Ezekiel alikuwa pia amehudhuria kwani alikuwa mkaribu wa wema sepetu aliyekuwa amealikwa kwa tamasha.

Musa Iyobo and aunty Ezekiel

Wakiwa huko afrika kusini, mose Iyobo na Aunty Ezekiel walianza mazoea hadi ikafikia kuitana mchumba. Baada ya kutoka south africa, wawili hawa walipoteana. Kwa bahati nzuri, Musa Iyobo na Aunty Ezekiel walikuja kupatana tena na hapo ndipo walibadilishana namba za simu.

Hapo ndipo walianza kukuza mahusiano yao. Kulingana na Musa Iyobo, Aunty Ezekiel ndiye aliyeanza kumtongoza Musa Iyobo. Huwezi amini, mapenzi yao yalichukua mkondo mpya kwa mda mfupi sana kwani kabla hata ya wiki moja, Aunty Ezekiel alipata uja uzito wake Musa Iyobo.

Wamekuwa kwenye uhusiano kwa miaka kadhaa kabla ya waharibifu kuingilia Kati. Wakati Musa Iyobo anaanza mahusiano na Aunty Ezekiel, tayari Iyobo alikuwa na mtoto na mwanamke mwingine anayefahamika kama mwengi. Kuna mda aunty Ezekiel walirushiana maneno na mwanamke huyu yote yakiwa ni uhusiano wao wa kimapenzi.

Musa Iyobo ilibidi aingilie Kati ya vita vya wanawake hawa wawili ili kuweza kutatua mzozo wao. Kulingana na yeye, mzozo wao ungeendelea ungeleta athari hata kwa watoto wa wanawake hawa wawili. Tunaweza kusema Musa Iyobo alifanya Kazi kubwa ya kuwapatanisha wawili hawa kwani baada ya hayo yote wawili hawa waliacha vita vyao ni Kuna wakati aunty Ezekiel na mwengi  walipiga picha pamoja.

Ndani ya kipindi Cha Lavi Davi kinachopeperushwa ndani ya wasafi F.M, mose Iyobo alieleza kuwa, Chanzo Cha kuachana kwa Musa Iyobo na Aunty Ezekiel ilikuwa ni marafiki wa Aunty Ezekiel waliokuwa wakimshauri vibaya.  Kulingana na Musa Iyobo, wenzake aunty Ezekiel hakuwa na mazoeana nao kwani tokea hapo mwanzo aliona kuwa sio watu wazuri.

Wenzake aunty Ezekiel walimfanya kumsaliti Musa Iyobo na inasemekana aunty Ezekiel alianza kutoka na wanaume wengine. Hayo ni machache tu kuhusiana uhusiano na Mose Iyobo na sababu ziliwafanya wawili hawa kuachana.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *