HistoriaMaisha

Historia ya willy Paul

Historia ya willy Paul ni ya kipekee kwani amepitia mengi sana kufikia hapo alipo. Ana majina kadhaa na wengi wanapenda kumuita Willy pozee. Willy Paul alizaliwa mwezi wa tisa mwaka wa 1993. Alizaliwa mtaa wa Mathare slums iliyoko mjini Nairobi.

willy Paul songs

Kwa sasa Willy Paul ni msanii mwenye bidii sana kwani anajua alipotoka na mahali amefika. Kusema kweli alipitia maisha magumu sana na kwa sasa anafurahia bidii yake.

Willy Paul alizaliwa na familia ya Radido wanaosemekana kutoka Tanzania na Uganda. Ina maana mzazi mmoja wake ametoka Tanzania na mwingine Uganda. Kabla ya kutoka kimziki, willy Paul alifanya Kazi ya juakali ili aweze kumlisha mamake aliyekuwa amelazwa. Wakati mamake Willy Paul akiwa mgonjwa, willy Paul ilibidi akatize masomo ili aweze kumshughulikia mamake.

willy Paul mother

Kwa mda sasa Willy Paul amekuwa kwa tamasha mbalimbali na ametembelea nchi nyingi ikiwemo U.S.A. Katika mashindano ya Groove awards, will Paul amepata tuzo nyingi wakati alikuwa anafanya mziki wa injili.

Nyimbo yake ya Rabuka ndio ilimfungulia njia. Nyimbo hii iliachiwa mwaka wa 2010 na baadae akafanya kolabo na Gloria Muliro nyimbo iliyojilikana kama ‘sitolia’. Nyimbo hii ilikuwa inaongelea maisha yake na aliweza kuelezea historia yake. Pia ilikuwa ni kama shukurani kwa mwenyezi Mungu kwa kuyabadilisha maisha yake.

willy Paul wife

Mnamo tarehe 5 December mwaka wa 2013, will Paul aliachia album yake ya kwanza iliyojilikana kama ” You never Know” uzinduzi wa album hii ulifanyika KICC na waliohudhuria ni Daddy Owen, Ben githae, Gloria Muliro, Dk Kwenye beat, Ben Bahati, Bahati, Men Of God (MOG), Size 8, Mr Seed, Shiru Wa GP, Betty Bayo, Danny Gift, DJ Sadic and DJ Mo.

 

Nyimbo zilizokuwemo katika album hiyo ni pamoja na colabo nyengine ya Gloria Muliro, “nitajitia kitanzi”, you never know, lala salama, mapenzi

Mwaka wa 2014, willy Paul alitangaza kufanya tour nchini marekani iliyodhaminiwa na talanta awards. March 10, willy Paul alitua ndani ya Sacramento California. Alipata nafasi ya kutumia ukumbi mmoja na Polly odotte wa The house of glory church.

Safari yake hikuishia hapo kwani pia alitembele kanisa ya Neema Gospel church iliyoko Dallas Texas. Mnamo march 15 alikuwa na tamasha nyengine ndani ya St Louisiana, Missouri. Kati ya 29 na 3Oth March, willy Paul alikuwa Neema community church iliyoko overland park Kansas. Safari yake ilifika kikomo tarehe 27 April ndani ya Las Vegas, Nevada.

willy Paul wife photos

Kuna mda willy Paul alikuwa na beef na bahati Kenya kwa madai kwamba Bahati alikuwa anamuibia nyimbo zake. Mashabiki wake bahati walimtetea kupitia mitandao. Hii beef yao haukuendelea sana kwani tarehe 22 April 2015 katika groove awards nominations, wawili hawa walitakikana kupeana mkono kama ishara ya kusameheana huku maombi rasmi yakifanyika ili kumaliza beef yao.

Nyimbo ya willy Paul na Size 8, “Tam Tam ilimuezesha kupata tuzo mbili za mdundo kama nyimbo ya injili iliyopakuliwa zaidi na msanii wa kiume bora. Tuzo zingine mbili alizozipata ni tuzo ya collabo of the year na pia best video of the year.

Kwa sasa Willy Paul anafanya secular music baada ya kudai kwamba walioko kwa mziki wa injili hawataki na hawampi nafasi katika gospel industry. Ashawahi Fanya kolabo na mkali wa mziki wa kufoka nchini kenya anayejulikana kama khaligraph Jones kwa nyimbo inayojulikana kama bora uhai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *