Sanaa

Msanii wa kenya afanya collabo na Lil Wyne

Sio wengi wangedhania kuwa msanii wa Kenya anaweza fanya colabo na msanii mkubwa Kama Lil Wyne. Japo sio rahisi wakati huu imeweza kufanyika

Talanta inaweza ikakupeleka sehemu zenye hujawahi kufika. Inaweza pia ikafanya ukututane na watu wakubwa kwenye sanaa. Huenda pia ujakujulikana ulimwengu mzima na mengine mengi.

Nikisema hivo haimanishi ni kitu rahisi. Unatakiwa ufanye bidii sana na pia uwe Mvumilivu. Kumbuka ni wengi sana wako na talanta kwa hivyo lazima uwe tofauti na wengine ndio uwe mshindi. Ina maana unatakiwa ufanye kazi ya ziada.

Msanii mmoja kwa jina mark mbogo kutoka Nairobi anasemekana kushirikishwa na msanii wa kufoka anayejulikana kama Lil Wayne katika album yake mpya inayojulikana Kama dubbed funeral.

Msanii wa kenya

Lil Wayne ameachia album yake mpya ya nyimbo 32. Wasanii wengine aliowashirikisha ni pamoja na Doja Cat, Like Uzi Vert, Tory Lanez, Adam Levine, 2 Chainz, take off, Bid Sean na wengine wengi.

Kaycyy Pluto ambaye jina lake halisi ni mark mbogo ameshirikishwa kwa track inayojulikana Kama Big Worm.

Kaycyy ni mkenya ila kwa sasa anaishi Atlanta, Georgia na Anajulikana kwa nyimbo kadhaa. Yeye pia ana jina maana kuna nyimbo zake ameshirikisha wasanii wakubwa Kama vile Lil Baby na Lil Keed

Kaycyy Pluto anapanga kuachia album ya pili hivi karibuni.

Soma hii pia (utajiri wa haraka)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *