Maisha

Utajiri wa haraka

Kila mwanadamu yupo mbioni kutafuta hela. Wengi wako tayari kufanya lolote ili kuwa matajiri. Je, swali ni kunao utajiri wa haraka.

Kulingana na utafiti wetu, utajiri wa haraka upo ila kuna vitu mingi hufuata unapopata utajiri wa haraka. Hili halitokei rahisi vile unavyofikiria ndio maana nikasema kuna watu wako tayari kufanya lolote ili waweze kupata hela.

Kuna watu Wana bahati sana na huenda wakapata pesa halali kwa mda mdogo sana bila kutumia njia za kihuni. Wao hufanya bidii ama Mara nyingine hubuni vitu ambazo Baadaye hutumika na karibia kila mtu dunia nzima.

Tamaza mtu Kama Billy Gates. Ni mwanzilishi wa Microsoft na utajiri wake ulipatikana kutumia ubunifu wa kipekee. Saa hii ana hela zake nyingi sana.

Bill Gates Microsoft founder
Billy Gates

Mwingine ni mark Zuckerberg. Huyu ndiye alianzisha mtandao wa Facebook na pia amenunua WhatsApp. Kwa sasa ni Kati ya matajiri wakubwa ulimwenguni.

 

Watu Kama hawa hupata baraka zake mwenyezi Mungu kwani utajiri wao haukupatikana kwa kula jasho ya mwingine ila bidii yao.

Kulingana na maoni yangu, ni vizuri kula jasho lako. Wakati mwingine usipopata pesa kwa njia halali basi ujue malipo ni hapahapa. Kuna wengi walipata utajiri wa haraka na kwa sasa familia zao zinapitia matatizo yenye hayawezi tatuliwa na hizo pesa.

Unaweza pata mtu ana magonjwa sugu na hata awe na pesa vipi, ile hela haisaidi. Wengine hata huaga dunia na kuacha zile hela. Cha ajabu ni kwamba wenye huachiwa hizi pesa huanza kupigana na huenda wakazitumia kwa njia isiyofaa na mwishowe wakawa maskini wa mwisho

Najaribu kusema kama unataka utajiri wa haraka fanya bidii Wala usitumie njia za mikato. Wakati wote unachofanya Jambo sahihi, Mungu naye atakubariki na huenda akaona bidii yako na akakutunuku hela ya kisawasawa.

Muombe mungu sana wakati wote na kila unachofanya Jambo fanya kwa uwezo wako wote na siku moja utaona matunda ya bidii yako.

Soma hii pia ( Vita baina ya vera Sidika na Otile Brown vyapamba moto)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *