MchipukoAfyaMaisha

Mwanaume wa miaka 80 afia hotelini akiwa na mwanamke wa miaka 33

  • Mwanaume wa miaka 80 afia hotelini akiwa na mwanamke wa miaka 33 
  • Inasemekana wawili Hawa wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi
  • Mwanamke huyo kwa jina neema kibaya amezuiliwa katika kituo Cha polisi

Mwanaume wa miaka 80 amefariki dunia kwa njia isiyoeleweka ndani ya nyumba ya starehe almaarufu guest house. Mwanaume huyu anasemekana kuwa na mwanamke wa miaka 33 usiku kutwa.

David Makerege amelipotiwa kufariki jumamosi tarehe kumi na sita. Mwanaume huyu alikuwa na msichana kwa jina neema kibaya.

Mwanaume wa miaka 80 afia hotelini akiwa na mwanamke wa miaka 33

David Makerege alipatikana amefariki ndani ya guest house chumba nambari 22 huko maeneo ya mbezi garden kwenye inasemekana alikuwa anajifurahisha nafsi yake na neema kibaya ambaye kwa sasa amekamatwa na askari na  kuzuiliwa katika kituo Cha polisi.

David Makerege na neema kibaya

Habari hizi zilitolewa rasmi na  kinondoni police commander ramadhan kingai.

” Polisi walifika kwenye tukio na kupata mwili wa david Makerege pamoja na mwanamke kwa jina neema kibaya. Neema alielezea askari kwamba yeye na mzee david Makerege wamekuwa kwa uhusiano wa kimapenzi kabla ya hilo tukio kufanyika…. Polisi walipashwa habari saa tisa usiku na wasimamizi wa hoteli ndio wakaamua kufika maeneo ya tukio…”

Polisi waliuchukua mwili wa mwendazake na kuupeleka hospitali ya mwananyamala kufanyiwa upasuaji ili wajue chanzo Cha kifo chake. Kulingana na polisi, huenda mzee david mluli alikufa kifo Cha kawaida maana hakuonekana kuumizwa sehemu yoyote ya mwili wake ila uchunguzi unaendelea.

polisi waliweza kupata pesa, kitabulisho chake na simu aina ya techno ndani ya hiyo room walimolala wawili hawa.

Soma hii pia ( huyu ndiye Babake diamond platnumz)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *