MchipukoSiasa

Uhusiano wa Uhuru kenyatta na william Ruto wazidi kudidimia

  • Uhusiano wa Uhuru kenyatta na william Ruto wazidi kudidimia
  • William Ruto ni naibu rais nchini Kenya
  • Uhuru kenyatta na william Ruto wamekuwa marifiki zaidi ya miaka saba.
  • William Ruto ana tofauti na aliyekuwa prime minister nchini Kenya Raila Odinga
  • William Ruto haungi mkono BBI ila Uhuru kenyatta na Raila Odinga wanaunga mkono BBI
  • William Ruto na Uhuru kenyatta waliwahi kufikishwa kwenye mahakama ya kimataifa.

Hakuna aliyetarajia wawili hawa wangekuja kuachana. Kumbuka william Ruto na rais Uhuru kenyatta wamekuwa pamoja kwa miaka mingi na kuungana kwao kulichangia kupata uongozi wa nchi ya Kenya.

William Ruto na Uhuru kenyatta waliwahi kushitakiwa katika mahakama ya kimataifa ila wawiliweza kushinda kesi na kuachiliwa. Kabla hata ya kesi yao, wawili hawa waliungana ili kuwa Kati ya wale waliogombea kiti Cha urais. Sio wengi walidhania wangepata kura kwa sababu ya kesi iliyowakabili.

Baada ya kura za mwaka wa 2013, Uhuru kenyatta alitangazwa mshindi naibu wake akiwa william Ruto. Baada ya miaka tano, william Ruto na Uhuru kenyatta walisimama tena na kupata ushindi tena.

Mwaka wa 2018 , tarehe tisa mwezi wa tatu, Uhuru kenyatta na Raila Odinga waliungana kwa nia ya kuunganisha wakenya almaarufu kama “handshake”. Muungano huu haukumfurahisha naibu wa rais william Ruto maana aliona bidii yake na Uhuru kenyatta Kupoteza nguvu na maana. Hapo ndipo BBI ikazaliwa na mambo yakazidi kukorogeka huku Ruto akionekana kuwa na utofauti kuhusiana na BBI.

Uhuru kenyatta Raila Odinga handshake

William Ruto aliamua kuanzisha kampeni kivyake baada ya kuanzisha husler team. Kulingana na Ruto, yeye anaamini wanainchi wa kawaida wako na umuhimu zaidi kuliko vyeo vya viongozi. Ruto alipata upinzani mkubwa sana kutoka chama Cha odm na chama kinachoongoza, jubilee.

William Ruto hakufa moyo na akionekana kuendelea na kampeni yake bila kujali wapinzani wake. Kwa mda, Ruto amekuwa akimtetea rais Uhuru kenyatta na serikali kwa jumla ila yeye na Raila Odinga wanaonekana kuwa na utofauti.

Unga ulizidi maji hivi majuzi kwenye mazishi ya mamake musalia mudavadi. Kila aliyeongea kwenye mazishi hayo alionekana kukerwa na william Ruto. Wengi walionekana kumuomba nafasi Uhuru kenyatta aweze kuchukua hatua dhidi ya naibu wake.

Uhuru naye alipopata nafasi ya kuongea kwa mazishi ya mamake musalia mudavadi, alionekana mwenye hasira na ikafikia hatua ya kumuongelea william Ruto japo kwa mafumbo. Uhuru kenyatta alisikika akisema kwamba ni wakati wa jamii nyengine kutawala nchi ya Kenya kwani tokea nchi ya Kenya kupata Uhuru, jamii mbili ndizo zimekuwa zikitawala.

Wanaomuunga mkono naibu wa rais william Ruto hawakufahia matamshi ya rais Uhuru na walitaka aombe msamaha. Ruto naye hakuachwa nyuma kwani yeye pia alionekana kushangazwa na matamshi yake Uhuru kenyatta ambaye amekuwa rafiki yake kwa miaka mingi. Ruto aliyeonekana kukerwa na matamshi hao alieleza umati kwamba hakumuunga mkono Uhuru kenyatta maana ni mkikuyu ila sababu ni kwamba aliona Uhuru ana uwezo wa kuiongoza nchi. Aliongeza na kusema kwamba siasa za ukabila zimepitwa na wakati na jamii zote zafaa kuungana.

Juzi Uhuru kenyatta akihojiwa kwenye radio alisema, haogopi lolote ama mtu yeyote na watu wasione simba amenyeshewa wakadhania ni paka. Aliongeza kuwa hatowatumia askari wakamatwe wanaomtukana kwani yeye ana kazi nyingi za wanainchi anazotakiwa kuzifanya.

Siasa nchini Kenya zimeshika moto na kusema kweli mwaka wa 2022 kutakuwa na kivumbi nchini Kenya. Cha kushangaza ni kwamba, wanasiasa wengi  wanaonekana kumvamia mtu mmoja ambaye ni naibu wa rais william Ruto. William Ruto ana wafuasi kwenye ngome ya Uhuru kenyatta kwani wenyeji wanadai kwamba Ruto alisaidia Uhuru kenyatta kupata urais. Kumbuka kuna wakati Uhuru kenyatta aliahidi kuongoza kwa miaka kumi alafu amuachie naibu wa rais william Ruto kiti hicho naye aendelee na miaka yake kumi. Sababu hizi na zingine ndizo zinazochangia wanainchi kutoka mkoa wa Kati kuonekana kumuunga mkono Ruto badala ya rais Uhuru kenyatta.

Kwenye upande mwingine Raila Odinga anaonekana kufurahia matunda ya handshake na kwa hivi sasa anafanya kampaini za BBI. William Ruto hadi sasa anapinga BBI huku akitaka viongozi waifanyie marebisho kama vile kupunguza nafasi za viongozi na kutoa ajira kwa mwananchi wa kawaida.

Hapa mwangaza letu ni jicho tu tukiyatazama matukio mbalimbali kwani Kila siku kunazuka mapya. Zidi kufuatilia habari zetu kutoka tovuti yetu ya mwangazanews ili tuweze kukujuza mengi zaidi.

Soma hii pia ( utajiri wa william Ruto)

Soma hii pia (utajiri wa Raila Odinga)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *