AfyaMchipuko

Rais pombe magufuli : Hakuna corona nchini Tanzania

Rais pombe magufuli amesema kwamba nchi yake imepigana na ugonjwa wa Corona virus na kwa sasa nchi yake imemaliza kabisa virusi vya coronavirus.

Ameongezea kuwa maombi imefanya kazi na Mungu amesikiza maombi ya nchi yake na kuiondoa coronavirus kabisa. Hii imefanyika wiki sita baada ya Tanzania kuacha kutangaza maambukizi ya corona Kama nchi zingine zinavyofanya.

“Huu ugonjwa umemaliza na nguvu za mungu… Alisema magufuli jumapili iliyopita kanisani moja mjini dar… Alisema rais pombe magufuli

Alipongeza waumini kwa kutovaa barakoa akiongeza kwamba Imani yao imesaidia sana katika kipigana na homa ya Coronavirus. Alizidi kuwahimiza wanainchi kutovalia barakoa zenye hazijaidhinishwa na shirika la afya nchini Tanzania.

magufuli ni mwana kwaya katika Kanisa katoliki. Wagonjwa wa Corona Mara ya mwisho kutangazwa nchini humo walikuwa 509.

wakati nchi nyingi za afrika zinapongezwa kwa jinsi wanavyopigana na ugonjwa wa Coronavirus, rais magufuli anasema kuwa ugonjwa huu hauko kwa wingi Kama vile unatangazwa ila unatumika kuharibu uchumi wa nchi. Rais Magufuli siku chache zilizopita alisema mwanawe alipona corona baada ya kunywa malimau.

Rais Magufuli aliwahi kuwafuta kazi wafanyi kazi wa shirika la afya ulimwenguni waliokuwa wanasimamia afya nchini Tanzania. Pia ni rais Magufuli  hajawahi funga hata sehemu moja nchini humo. Wanainchi Tanzania wako na uhuru wa kutembea kila sehemu ya nchi.

Rais pombe magufuli

Wakati magufuli aliingia kwa mamlaka, kuna msimamizi wa afya aliwahi kutangaza kuna homa ya “zika virus”. Rais Magufuli alimfuta kazi na tangu hiyo siku hakujawahi kesi yoyote ya homa ya Zika virus.. alisema magufuli wakati alipokuwa anaongea na waalimu mjini Dodoma.

“Waliwahi kusema kuna ebola ili wazuie watali kuja hapa Tanzania na hakuna aliyekufa kwa ebola….kwa sasa ni corona, walisema maiti zitatapakaa barani afrika hawakujua mungu yupo na anaipenda nchi ya Tanzania.. tumefanya maombi siku tatu na kwa sasa hakuna corona nchini Tanzania.

Alitangaza kuwa watu wanne peke yao ndio Wana virus ya corona Kati ya watu million sitini nchini Tanzania.

Soma hii pia ( je, William Ruto ana nafasi ndani ya jubilee)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *