MchipukoUhalifu

Roxie Washington Mkewe George Floyd na mwanawe waongea kwa mara ya kwanza

Hata kabla ya kuanza kuongelesha umati uliokuwepo mineapolis city hall, Roxie Washington alionekana mnyonge na machozi yalimjaa machoni. Alikuwa pamoja na mwanawe wa kike Gianna.

” Niko hapa kwa ajili ya mme wangu George na mwanangu Gianna…. Hayo ndio yalikuwa maneno yake kabla ya kuangua kilio. Tokea bwanake George Floyd afe, hii ni mara ya kwanza kwa Roxie Washington kuongea hadharani. George Floyd alifariki tarehe ishirini na tano.

Floyd mwenye miaka 46 alihamia Minnesota kutafuta kazi na kwa bahati nzuri alipata kazi ya dereva wa truck. Alikuwa anakaa Houston kabla hajahamia Minnesota. Hakufanya kazi ya udereva tu kwani pia aliwahi kuwa mlinzi katika kampuni ya Conga Latin Bistro.

Roxie washington Gianna George Floyd

Floyd alikuwa akiwasaidia familia yake kwani akiwa kazini alikuwa akimtumia mkewe pesa za matumizi huko Houston walimokuwa wanaishi. Wakati huo Gianna ambaye ni mtoto wao wa kike alikuwa bado mdogo.

Mnamo tarehe ishirini na tano mwezi may, Floyd aliuliwa baada ya kukabwa koo na goti huku akiwa amefungwa pingu na polisi wa Mineapolis. Derek Chauvin ndiye polisi aliyemfinya koo kutumia goti lake kwa mda wa dakika tisa. Inasemekana Derek Chauvin na wenzake watatu walikuwa wanamtafuta Floyd kwa makosa ya mahesabu ghushi ya dola $20. Kwa sasa polisi hao watatu waliweza kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

George Flyod

Roxie Washington anasema Floyd alikuwa amelala wakati Roxie alikuwa anajifungua Gianna na aliamushwa na kilio cha gianna alipozaliwa.

“Nasikitika Gianna hatawahi kumuona babake tena na kama kuna kitu alikuwa akipate kupitia babake, basi hana bahati maana hatawahi pata…”Alisema Roxie Washington tazama video hapa chini

Soma hii pia ( Wenye ndoa wanatakikana kuvaa Mask wanapofanya tendo la ndoa)

 

 

 

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *