Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen atetea hatua yake ya kuondoka mkutano wa BBI kabla kukamilika
Seneta Kipchumba Murkomen amejitetea vikali kuhusiana na tukio lililofanyika Meru katika mkutano wa BBI. Murkomen amesema alikuwa na dharura na hangeweza kukaa zaidi kwani alikuwa anahitajika sehemu nyengine.
Murkomen na Moses kuria walipofika walikosa mahali kwa kukaa na walieza kusimama kwa mda kabla ya kutafutiwa viti. Wakaazi wa Meru walilalamika na kutoa kauli Kali kuwa lazima Murkomen angepewa nafasi ya kuongea na wanainchi.
Maombi yao yalisikizwa na Murkomen akapata nafasi. Murkomen aliwashukuru wakaazi wa Meru kwa kumchagua Uhuru Kenyatta na William Ruto katika uchaguzi uliopita.
Aliwahimiza wanainchi wasikubali kutapeliwa na wajue haki yao.
1,111 total views, 1 views today