Afya

Siri ya urembo wa uso 

Kama utakuwa hauna ufahamu na Siri ya urembo wa uso, basi kila siku utakuwa wauliza mungu maswali ambayo hayana msingi. Kwa Mfano, ukichelewa kulala basi jua asubuhi macho yako yakuwa yamezungukwa na alama nyeusi. Hii sio mambo na maumbile Ila ni kutofahamu Siri ya urembo wa uso

Kabla hujalala hakikisha umeoga uso ili kutoa vipodozi vya aina yoyote uliyotumia mchana kutwa. Ngozi ya binadamu inafaa kupumua na kupata hewa Safi sanasana usiku wakati umelala. Kama utakuwa hujanawa uso vizuri basi utazuia hewa Safi kupata nafasi ya kuingia ndani ya ngozi.

Unahimizwa kutotumia chemical yoyote kutoa vipodozi usoni kwani huenda ukaleta madhara zaidi. Unatakiwa utumie maji ya kawaida na sabuni ama pia unaweza tumia pamba na mafuta ya olive oil.

Chakula unayoitumia pia inachangia sana urembo wa uso. Unatakiwa kula matunda mboga na chakula yenye protein na vitamins. Chakula yenye iko na vitamin C na isiwe na mafuta mengi husaidia sana ngozi ya binadamu sanasana uso.

Pia hakikisha hautumii sukari nyingi ndio kiwango Cha insulin kiwe chini na hii itachangia ngozi yako kuwa na afya. Chakula chengine unafaa kuepukana nacho ni chakula chenye viuongo vingi kama vile pilipili pia punguza kiwango Cha chumvi. Chakula Cha mafuta mengi pia sio kizuri ikiwezekana kula chakula Cha kuchemshwa kama vile wali.

Tukiongelea Siri ya urembo wa uso tunafaa kuelewa kwamba mazoezi pia ni mhimu sana. Unapofanya mazoezi kama vile kukimbia husaidia sana kuiwezesha damu kuwa na urahisi wa kuzunguka mwilini. Hii pia itakufanya utokwe na jasho ambayo pia ni njia moja ya kusafisha mwili. Kumbuka sio lazima ukimbie sana. Kwa wale waoga wa kuchoka kwa kukimbia, hata kuizunguka nyumba yako pia ni mazoezi yakutosha sanasana kama jasho itakutoka

Kama wataka ngozi yako iwe laini na ya kupendeza, basi inatakiwa ulale usingizi wa kutosha. Sisemi uanze kulala tu bila kufanya Kazi Ila tu uhakikishe umelala masaa ya kutosha. Kila siku unafaa kulala masaa nane. Kama hautapata usingizi wa kutosha, ngozi yako itaanza kulegea na utakaa kama umechoka. Ni vizuri pia kupaka uso wako asali Mara mbili ama tatu kila wiki. Hii husaidia kufanya uso wako uwe laini na pia huponya hitilafu ndogondogo kwenye uso.

Katika Siri za urembo, maji pia ni mhimu sana. Unatakiwa kunywa maji kwa wingi sana. Sio tu wakati umekula chakula Ila pia wakati unaendelea na Kazi zako za kila siku. Unaweza pia ukala matunda ama mboga zenye zina maji mengi kama vile tikiti maji, cabbage, machungwa na zinginezo.

Osha uso na maji moto Mara tatu kwa siku. Kama unatumia miwani hakikisha pia unaisafisha ili kutoa mafuta ama vipodozi vilivyotumika hapo awali. Jihadhari sana na msongo wa mawazo kwani huenda ukachangia pakubwa kuharibu urembo wako.

Kama itawezekana jaribu kwenda matembezi ili utoe fikira zenye huenda zinakusumbua. Wakati unakuwa na msongo wa mawazo, mwili wako hutoa kemikali inayojulikana kama cortisol na homoni zingine zinazofanya ngozi yako iwe na mafuta zaidi.

Kwa sasa nina uhakika unaelewa machache kuhusiana na Siri za urembo wa uso pamoja na urembo wa ngozi yako. Asanteni kwa kufuatilia habari zetu hapa mwangaza news.

Soma hii pia: umuhimu wa kufanya tendo la ndoa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *