Mchipuko

Tazama vazi alilovaa Gigy money na kusababisha wasafi Tv kufungwa

Tazama vazi alilovaa Gigy money na  kusababisha wasafi Tv kufungwa..

Taarifa zinazogonga vichwa vya habari kwa sasa ni kuhusiana na kufungwa kwa wasafi Tv. Tume ya TCRA inayoshughulika na mawasaliano nchini Tanzania imeifungia wasafi Tv kutorusha matangazo kwa mda wa miezi sita.

Gigy money pia amejipata pabaya maana pia yeye alifungiwa miezi sita kutofanya tamasha yoyote ile na kutakiwa kulipa faini ya milioni moja. Hii ni Mara ya pili kwa wasafi kufungiwa maana miezi michache iliyopita waliwahi kufungiwa kituo chao Cha radio kwa siku saba baada ya kupeperusha matangazo iliyokiuka maadili ya kijamii.

Kwenye tamasha lilopeperushwa moja kwa moja na wasafi Tv, msanii Gigy money alipanda kwa stage akiwa amevalia Dera ila alipofika aliivua ile Dera na kubakia na nguo zilizosemekana kukiuka maadili ya kijamii.

Gigy money na wasafi Tv wafungiwa

Baada ya tukio hiyo, tume ya TCRA iliamua kuchukua hatua Kali kea runinga ya wasafi na kuwaonya vikali.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *