MchipukoSanaa

Ugomvi wa master Jay na S2kizzy wachukua mkondo mpya

Sanaa ya tanzania haikosi vituko kila uchao, kwa sasa jipya ni kwamba, Ugomvi wa master Jay na S2kizzy wachukua mkondo mpya.

Kumekuwa na sitofahamu baada ya kile alichokiandika master Jay kwenye Instagram page yake. Master jay alisemekana kumlenga S2kizzy kwa mienendo yake.

Master jay alidaisha kwamba producers wengi wa Tanzania ni kama Chawa. Inasemekana S2kizzy huzunguka kwa wasanii tofauti tofauti bila hata kujali kuingiza hela mfukoni. Kulingana na master jay, producers wa siku hizi hawajali pesa Ila wanataka tu kuwa na majina makubwa.

Kwa sasa Ugomvi wa master Jay na S2kizzy wachukua mkondo mpya na huenda wawili hawa wasielewane kwa mda Ila tunawaombea wawili hawa wakutane waweze kuyatatua mambo yao.

Akiongea na wasafi media master jay alisema producers wako na rights za kulipwa kama nyimbo inapata kuchezwa kwa media Ila kwa sasa hela yote inaenda kwa msanii. Master jay aliongeza kuwa sio kwamba anawadharau Ila anajaribu kuwaelimisha.

S2kizzy kwa upande wake alikanusha kuwa wao ni kama Chawa huku akisema kwa sasa wanalipwa vizuri kuliko hapo awali wakati wake master jay. S2kizzy alisema producers wengi wa Tanzania kwa sasa wamamiliki magari, mashamba na vitu mingi vya dhamani.

Kulingana na S2kizzy, wakati producer anapo safiri na msanii huwa anapata marupurupu zaidi. Hiyo Ina maana wakati S2kizzy anapoonekana na wasanii kama vile diamond platnumz, watu waelewe kuwa anaingiza hela zaidi na sio eti yeye ni Chawa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *