MaishaMchipuko

Ugomvi wa wema sepetu na Zari Hassan

Najua Kuna wengi sana wanawafahamu wanawake hawa wawili lakini sio wengi wanajua mengi kuhusiana na Ugomvi wa wema sepetu na Zari Hassan

Ni wanawake wawili ambao wako na historia kwenye uhusiano wa kimapenzi na diamond Platnumz. Wema sepetu ndiye alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa na diamond japokuwa hakufanikiwa kupata watoto.

Wakati Diamond platnumz hajaanza kujulikana alipatana na wema sepetu wakati huo wema sepetu alikuwa miss tanzania. Walianza urafiki na kupitia kwa wema sepetu Diamond platnumz alianza kujulikana kwani tayari jina la wema sepetu lilikuwa juu sana.

Uwepo wa wema ulichangia sana Sanaa ya Diamond platnumz na hapo ndipo nyimbo za diamond zilianza kujulikana hata nchi za nje. Wawili hawa waliingia kwa mapenzi na kuanza kuishi pamoja.

Baada ya kujaribu kwa Mara nyingi, hawakuweza kupata mtoto. Ni wakati huohuo zari Hassan na diamond walianza uhusiano wa kimapenzi. Hapo ndipo wema sepetu aliwekwa kando baada ya diamond platnumz kujishindia mpenzi mpya kutoka nchi jirani ya Uganda.

Diamond platnumz na zari Hassan walifanikiwa kupata watoto wawili, akiwemo Tiffah ambaye kwa sasa ni maarufu sana katika mitandao. Kutokea hapo ndipo ugomvi wa wema sepetu na Zari Hassan ulipoanzia. Nakumbuka hivi majuzi zari Hassan aliwahi kumwambia wema sepetu atafute chakula angalau mwili wake unawiri.

Wema hakutaka kujibizana naye kwani alisema hana mda huo. Zari Hassan ni mwanamke anayejiamini sana na haogopi chochote. Mwanamke huyu ana nguvu hata ya kujibizana na shabiki kwenye mitandao. Cha ajabu ni kwamba, katika wale wanawake ambao diamond platnumz ashawahi kuwa nao, zari Hassan ndiye anayependwa sana na mamake diamond platnumz.

Kumbuka Diamond kwa sasa amezaa na wanawake watatu tofauti akiwemo Hamisa Mobetto kutoka Tanzania na tanasha Donna Oketch kutoka Kenya. Kati ya wanawake hao wote, zari Hassan ndiye aliyeishi na Diamond kwa miaka mingi. Huenda zari Hassan anamuogopa wema sepetu kujishindia diamond platnumz tena.

Kwa sasa Diamond platnumz anadai hana mwanamke yeyote kwa sasa huku akidai kwamba ako kwenye mikakati ya kutafuta mpenzi mpya. Ugomvi wa wema sepetu na Zari Hassan haunokani kuisha Leo na huenda wawili hawa wasiwahi elewana. Japo Diamond platnumz na zari Hassan hawako pamoja, hukutana sana nchini afrika kusini kwa Mara nyingi sana.

Hapa mwangaza news hatuna mengi Ila kufuatilia habari na kama kawa kila siku tutakuwa wa kwanza kuwapa habari za hapa na pale.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *