MaishaMchipuko

Uhusiano wa Tanasha na Diamond wachukua mkondo mpya

Katika vile mambo yanavyokwenda, kuna uwezekano ya maneno yanayosemekana kwamba Uhusiano wa Tanasha na Diamond wachukua mkondo mpya.

Wawili Hawa walikuwa hawaongeleshani kwa sana na labda walipeana nafasi na Kila mtu alikuwa anafanya mambo kivyake. Siku chache zilizopita, wawili hawa walieka mawasaliano yao wazi baada ya Tanasha Donna kumsifia babake mtoto wake ambaye ni diamond. Diamond naye kwa upande wake aliweza kumjibu kupitia instagram comment ambapo sio kawaida yake.

Kuna mda Tanasha alidai kuwa anamlea mtoto wake pekee yake bila usaidizi wa babake ila kwa sasa mambo ni tofauti. Tanasha kwa sasa anasema uhusiano wake na diamond hauko vibaya kama vile watu wengi wanavyofikiria kwani wawili hawa wanamlea mtoto wao kwa pamoja.

Katika instagram post yake Tanasha alimsifia Diamond Platnumz kwa kumtoa kimziki na kumsaidia kwa njia nyingi. Tanasha aliongezea kuwa nyimbo yake na diamond “gere” ndio iliyomfanya kujulikana ulimwengu mzima. Diamond naye alimtupia emoji za kuonyesha kuwa anamkubali mwanadada huyu na kumuhimiza kuendelea kufanya bidii.

https://www.instagram.com/p/CJrb2zVMtJo/?igshid=1cdkxw7u7cezn

Wawili Hawa walikuwa wapenzi na kuzaa mtoto pamoja ila kwa sasa waliachana na kila mtu anaishi kivyake huku Tanasha akiachiwa jukumu la kumlea naseeb jnr ambaye ni mtoto wao.

instagram ya Tanasha ujumbe kwa Diamond

Wote wawili hakuna ambaye ametangaza kuwa na mpenzi mpya na yaonekana labda mda bado. Ni hivi majuzi tu Zari Hassan aliyekuwa mke wa diamond aliwaleta watoto wake ili wakutane na baba yao. Sasa sijui kama naye Tanasha atapata nafasi kama ile ama hiyo nafasi iliwekewa Zari Hassan peke yake.

Mama dangote ambaye ni mamake diamond huonekana kumpenda Zari zaidi kuliko wanawake wengine ambao washawahi kuwa na kijana wake ambaye ni Diamond. Huonyesha kumchukia hamisa Mobetto zaidi na haijawahi kumpost mtoto wa hamisa Mobetto hata siku moja.

Video ya ney Mitego yazua gumzo _ tazama hapa

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *