Maisha

Utajiri wa Rihanna Kulingana na Forbes

Utajiri wa Rihanna Kulingana na Forbes; Msanii wa marekani anayejulikana kama Rihanna ameingia kikundi bilionea kwa sana inasemekana ni miongoni wa wanamziki tajiri wa kike duniani, kulingana na Forbes.

Rihanna ni msanii anayeheshimika sana na anafanya mziki aina ya pop. Kwa sasa unakisiwa kuwa ana utajiri wa Dola bilioni 1.7 hiyo ni kama pauni bilioni 1.2. inasemekana kampuni yake ya vipodozi ya Fenty beauty Ina thamani ya dol bilioni 1.4. Kulingana na Forbes, kampuni ya Fenty beauty ndio imechangia Rihanna kuwa bilionea.

Utajiri wa Rihanna Kulingana na Forbes

Utajiri zaidi pia umetokana na kampuni ya mavazi ya ndani inayojulikana kama savage x Fenty ambayo dhamani yake ni Dola milioni 270. Pia Rihanna anapata mapato mazuri kwa mziki wake na pia ni muigizaji.

Kwa sasa Rihanna ameshikilia nafasi ya pili kwani Oprah Winfrey bado anashikilia nafasi ya kwanza ya mwanamke tajiri duniani.

Kampuni ya Fenty beauty ilizinduliwa mwaka wa 2017 na Rihanna ambaye Jina yake kamili ni Robyn Fenty. Ina maana jina ya kampuni yake ilitokana na jina lake la kwanza. Hakuanza yeye tu kwani kulikuwa na ushirikiano wa kampuni ya bidhaa za kifahari LVMH.

Wakati wa uzinduzi wa Fenty beauty, Rihanna alisema lengo la kampuni yake ilikuwa kuzindua zaidi ya vipodozi ili aweze kuwavutia wanawake mbalimbali. Vipodozi hizi zilikuwa ni mpya kabisa kwenye biashara na ilikuwa ni Mara ya kwanza kuwahi kutokea.

kampuni yake ilifanikisha kampuni zingine kuweza kupanua soko lao kwa kuongeza Aina nyingi za vipodozi.

Kulingana na LVMH, Kwa mwaka wa kwanza baada ya kampuni ya Fenty beauty kuanzishwa, kampuni hiyo ilileta mapato ya zaidi ya Dola milioni 550 na hii iliendelea kwa miaka kadhaa

Rihanna ako na biashara zingine Ila sio zote zinazomletea mapato mengi kama kampuni yake ya Fenty beauty. Ni hivi majuzi msanii huyu maarufu alikubalia LVMH kufungua Lebo yake ya Fenty. Hii ni baada ya miaka ya utengenezaji wa nguo za kimitindo ama fasheni.

Rihanna ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 33, ameuza zaidi ya rekodi zaidi ya milioni 250 hiyo ni kabla ya mwaka wa 2016 kwani tangu huo mda hajatoa album nyengine

Hiyo ndio taarifa kamili kwa sasa kuhusu Utajiri wa Rihanna Kulingana na Forbes

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *