Afya

UFAHAMU UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS

UFAHAMU UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS DISEASE),VISABABISHI VYAKE NA TIBA YAKE

VIDONDA VYA TUMBO NI NINI???

Vidonda vya tumbo ni matokeo ya kuharibika kwa uteute wa ndani ya ukuta wa tumbo la Chakula au ndani ya utumbo mdogo wa Chakula na matokeo yake ni ukuta wa tumbo kugusana na tindikali iliyoko tumboni ambayo ni kali sana kama maji ya betri.
_vidonda vya tumbo husababishwa na maambukizi ya bacteria waitwao HELICOBACTER PYLORI, aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non_steroids anti inflammatory drugs kama vile ASPIRIN /DICLOFENAC huweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu.
_vidonda vya tumbo vinaweza kujitokeza katika utumbo mdogo na katika tumbo la Chakula na pia ni Mara chache huweza kujitokeza katika koo la Chakula ambapo hapakukusudiwa kustahimili tindikali ya tumbo

AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS DISEASE)

Kuna aina nyingi za vidonda vya tumbo tumeweza kufanya utafiti wa kina navyo ni
(a) vidonda vinavyotokea katika mfumo wa Chakula yani tumboni
b) vidonda vinavyotokea katika utumbo mdogo
(c) vidonda vinavyotokea katika koo /koromeo la Chakula
HATUA KUU ZA VIDONDA VYA TUMBO
ni vizuri kufaham kwamba huu ugonjwa una hatua nne ambazo ni muhimu
(1)HATUA YA KWANZA ~hatua ya kwanza ya huu ugonjwa ni ule uvimbe sugu unaotokea sehemu ya ndani ya tumbo,
(2)HATUA YA PILI~hapa vijidonda hujitokeza sehemu zenye uvimbe na taratibu vidonda hivyo huongezeka na kuwa vikubwa katika hatua hii mgonjwa hupatwa na maumivu makali ya tumbo yanayodumu kwa muda mrefu yakiambatana na kiungulia, tumbo kujaa gesi, kukosa hamu ya kula, choo kuwa kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu. Hata hivyo Hali hii ya kukosa choo kwa muda mrefu (CHRONIC DYSPEPSIA) yaani kushindwa kufanya Kazi kwa mfumo wa mmeng’enyo wa Chakula, kutokana na tindikali nyingi inayozalishwa tumboni huingia Kwenye mzunguko wa damu hivyo mgonjwa hujisikia uchovu na kizunguzungu cha Mara kwa Mara. Katika hatua hii tindikali husababisha magonjwa ya ini na Figo kwa kuwa tayari iko katika mfumo mzima wa damu
(3)HATUA YA TATU ~hii ni hatua ambayo ni ya hatari kwasababu vidonda vikubwa hupasua mishipa midogomidogo ya damu na kusababisha damu kuvia tumbon na kubadilisha rangi ya choo kuwa siyo ya kawaida, pia damu nyingi ikivujia tumboni mgonjwa hutapika na kuharisha damu. Hali hii husababisha mgonjwa kuishiwa damu Mara kwa Mara, maumivu makali ya tumbo,hupata Homa, maumivu ya viungo na kukosa hamu ya kula.
(4)HATUA YA NNE ~katika hatua hii saratani ya utumbo inahusika kwani katika hatua hii vidonda vya tumbo hutengeneza tundu katika tumbo au utumbo mdogo na kusababisha kuoza kwa viungo vya ndani na matokeo yake ni saratani ya utumbo

VISABABISHI/VIHATARISHI VYA VIDONDA VYA TUMBO

visababishi vya ugonjwa huu vipo vingi sana hivyo yatupasa kuviepuka ili kujiepusha na ugonjwa huu. Zifuatazo ni visababishi vya ugonjwa huu
i. Utumiaji wa madawa ya kuondoa maumivu kwa muda mrefu
ii. Mawazo na huzuni kwa muda mrefu
iii. Kutokuwa na muda maalum wa kula
iv.Utumiaji wa pombe uliopitiliza
v. Utumiaji wa madawa ya kulevya nk

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO

dalili na tiba ya vidonda vya tumbo
~Dalili za vidonda vya tumbo ni nyingi ila sio wote wanaopata Dalili hizi Wana vidonda vya tumbo
i. maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (EPIGASTIC PAINS)
ii. kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi Hali hii huweza kuendana na kucheua na kujamba Mara kwa Mara
iii. kutapika damu
iv. mtu mwenye vidonda vya tumbo (gastric ULCERS) hupata maumivu makali pindi anapokula au amalizapo kula
v. mtu mwenye vidonda vya tumbo katika utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali pindi anapokua na njaa.
vi. kupoteza hamu ya kula
vii. kupungua uzito

MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU

~matibabu ya ugonjwa huu yanapatikana vizuri nchini mwetu ila tatzo ni tiba yenyewe kutokua na wataalamu wa kutosha wa kutibu chanzo cha tatizo na kumaliza tatizo pasipo kuleta matatzo mengine kutokana na matibabu yenyewe kuhusisha mfumo wa dawa za kemikal ambazo Zina madhara kwa mhusika. Hivyo tiba bora kwa vidonda vya tumbo ni mlo kamili na dawa zisizo na kemikal pia tunapaswa kuepuka baadhi ya vyakula na kuzingatia masharti

MAMBO YA KUFANYA KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO

i. epuka kula vyakula vyenye viungo vingi kama vile pilau
ii. epuka kutumia pombe
iii. epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi
iv. kula Chakula kidogo kwa muda maalum
v. kula vyakula vyenye fiber yan vyakula vyenye nyuzunyuzi ambavyo ni jamii ya mbogamboga na matunda
vi. epuka unywaji wa kahawa au kinywaji chochote chenye caffeine kiepuke

Soma hii pia ( chakula inayoengeza damu mwilini)

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *