Maisha

Wasanii bongo Freemason

Ni swala ambalo huzungumuziwa sana nchini tanzania na ulimwengu kwa jumla ila swali letu ni, je kuna wasanii bongo freemason?. Kulingana na utafiti wetu, Wengi huamini kwamba msanii akifanikiwa ni lazima awe ni wa freemason. Kama unakumbuka kanumba, wengi walimuongelea sana na kusema alikuwa mmoja kati ya wasanii bongo freemason.

Ile sinema yake ya devil kingdom aliyoifanya pamoja na Ramsey Nouah ilizua maswali chungu nzima ikizingatiwa baada ya hii sinema haikuchukua mda kabla ya msanii huyu wa filamu kuaga dunia. Hapa mwangaza news hatuwezi sema kwamba sinema hii ndio ilikuwa chanzo ya kifo chake kwani bado tunaamini chanzo cha kifo chake ilikuwa ni ajali.

Devil kingdom Ramsey Nouah steven Kanumba

Wasanii wengine watanzania wenye huhusishwa na freemason ni wasanii wote wanaoonekana kufanikiwa katika mziki. Wasanii hao ni kama diamond platnumz na wenzake. Lakini kwa nini watu humshuku diamond platnumz kama mmoja wa wasanii bongo freemason?. Diamond platnumz ni msanii ambaye ana bidii sana katika kazi yake. Kama utakubaliana na mimi, ili ufanikiwe katika kila jambo, lazima utie bidii. Nachoamini ni kuwa bidii ya msanii huyu ndiyo inayoleta mafanikio ila sio mambo na freemason.

Diamond wasanii bongo freemason

Kafara za Freemason

Katika utafiti wetu, husemekana unapojiunga na freemason lazima uweze kutoa kafara. Kafara za freemason husemekana kuwa lazima utoe mtu wako wa karibu. Hii ndio sababu nikasema Kanumba na diamond huenda wasiwe wahusika wa freemason kwani hamna chochote kama hicho kishatokea kwa familia zao. Na kama nilivyotangulia kusema, utajiri wao ni kwa sababu ya bidii yao.

Pete za freemason

Kuna pete husemekana kuwa ni inshara ya freemason. Pete hizi husemekana kuwa tofauti na pete za kawaida na wengi husema pete hizi huvaliwa na wasanii au watu wenye majina tajika. Kuna wasanii huchukulia jambo hili kama la kutishia watu ili waweze kuogopewa. Wasanii hawa hutafuta mapete za kiainaaina na tofauti ndio watu wawaogope. Mara nyingi hizi pete hazihusiani na chochote kuhusu freemason ila vitisio tu.

zinazodaiwa kuwa pete za freemason
zinazodaiwa kuwa pete za freemason

Waimbaji wa Injili freemason

Imefikia hatua mpaka kukawa na maneno kuwa kuna watu hujificha na nyimbo za injili ila wao ni wasanii wa freemason. Kulingana na maoni yetu, hii sio rahisi kwani unapochagua shetani basi shetani mwenyewe anataka umtumikie yeye peke yake. Usisahau Mungu wetu aliyetuumba pia hapendi kuchanganywa na maovu kwa hivyo mpaka uwe na msimamo wakati unapochagua dini ama unapochagua mwenye utatumikia.

Freemason Tanzania

Nchi ya tanzania huonekana kuadhiliwa sana na mambo ya freemason. Kulingana na maneno ya watu, Wengi hata husema kuna makanisa na wachungaji wa freemason. Mpaka sasa hakuna anayeweza kutoa orodha ya makanisa hayo ama wachungaji wa freemason. Je huenda ikawa ni maneno tu na hakuna ambaye ana uhakika wa hili jambo. Wengi hutumia mitandao na kueleza jinsi ya kujiunga na freemason bure ila wengi wao ni walaghai na hakuna lolote wanaelewa. Baada ya kuwafutilia utajua mwishowe wanataka pesa zako tu na hakuna cha maana wanajua kuhusiana na freemason. Freemason inasemekana kuwa na siri nyingi na pia wana namba za siri. hii ina maana ukiona mwenzako anajidai kuelewa kuhusiana na freemason, basi muongo wa kwanza.

Freemason symbols

Je, kuna freemason Bongo

Kufikia sasa, hakuna mtu anaweza jibu hili swali. Hii ni kwa sababu sio wengi wanaweza kutoa mfano wa ni nani ama ni wapi tunaweza patana na hawa watu wa freemason. Kama nilivyotangulia kusema, ili uwe kwa freemason kuna kafara hufanyika na sanasana huwa za watu wa karibu na hizo familia zilizojiunga na freemason. Hii ina maana sio kiraisi vile wengi wanafikiria. Hapa mwangaza news bado hatujapata taarifa kamili kuhusiana na ninani ama ni wapi tunaweza wapata hawa watu wa freemason.

Ukiona mtu kafanikiwa, haimanishi kuwa yeye ni mmoja wa freemason ila labda ni bidii yake iliyomfikisha pale alipo. Wakati mwingine tuache kuona kama freemason ndio pekee inaweza ukufanya uwe tajiri, Usisahau kuna Mungu pia ambaye amewasaidia wengi sana na maisha yao kwa sasa imenyooka kwa sababu ya bidii yao

Soma hii pia ( wasanii matajiri Bongo)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *