Sanaa

wasanii wa Bongo

Tunapoongelea kuhusu wasanii wa bongo, ni lazima tumtaje msanii mmoja anayesemekana kuwa msanii tajiri nchini tanzania. Diamond platnumz ni msanii tajika na jina lake limeiwezesha nchi nzima ya Tanzania kujulikana ulimwengu mzima. Wasanii wa bongo wanajivunia uwepo wa diamond platnumz kwani bila yeye wangekuwa wanajulikana bara afrika ama afrika mashariki pekee.

Kama kuna wasanii wana talanta afrika mashariki, ni wasanii wa bongo. Hata kama wengine hawajulikani sana, ukiskia sauti zao utakubaliana na mimi kuwa wanaelewa mziki. Nitawataja wasanii kadha wa bongo na maelezo mafupi kuwahusu.

Diamond platnumz

Rayvanny and diamond wasanii wa tanzania

Ni msanii anayejulikana ulimwengu mzima. Amefanya kolabo na wasanii wengi wa kimataifa kama vile, Rick Ross, Neyo, Fally Ipupa, Davido na wengine wengi. Msanii huyu hufanya show za kimataifa na ili aweze kufanya show yako, basi hakikisha umejipanga kwani yeye huhitaji hela ndefu. Ana kampuni yake inayojulikana kama Wasafi ama ukipenda WCB. anamiliki recording label na runinga ya Wasafi T.v. Ana wasanii aliyowasajili kwa recording label yake. Wasanii hao ni kama Rayvanny, Mbosso, Lavalava, Zuchu na wengineo.

Alikiba

alikiba new song

Ni msanii anayependwa sana nchini Tanzania. Wengi humshindanisha na Diamond. Mashabiki wake huamini kuwa yeye ana uwezo mkubwa wa mziki kuliko diamond platnumz. Mziki wake husemekana kudumu zaidi kuliko mziki wa diamond platnumz. Amekuwa kwa mziki kwa miaka zaidi ya kumi na Tano na tunaweza sema anajitahidi sana kwani mpaka leo wengi wanaskiza mziki wake. Tofauti yake na diamond ni kwamba yeye haachilii nyimbo nyingi kwa haraka ila anapoachia nyimbo huipa mda ili iweze kupenya kabla ya kuachilia nyimbo mpya.

Harmonize

Harmonize and his wife Sarah
Harmonize na mkewe Sarah

Harmonize ni msanii anayejiamini sana. Msanii huyu alikuwa amesajiliwa wasafi ila aliamua kujitoa baada ya kuamini kuwa ana uwezo wa kuanzisha label yake. Kabla ya kuaga label ya wasafi, Harmonize alitakiwa kulipa kiwango cha pesa flani ili kuvunja mkataba wake na wasafi. Ilimlazimu kuuza nyumba zake kadhaa ndio aweze kulipa ile deni. Kwa sasa ako na label yake kwa jina Konde Gang. Kwa sasa ana msanii mmoja aliyemsajili kwa jina Ibra. Juzi alitangaza kusajili wasanii wengine hivi karibuni. Kulingana na habari za hapa na pale, Harmonize huenda akamsajili Mavoko. Kumbuka Mavoko aliwahi kuwa chini ya wasafi records kabla ya kutoelewana na label ya wasafi.

Mbosso

Mbosso Msanii wa Tanzania

Ni msanii amabye ana uwezo mkubwa sana. Anajua kuandika nyimbo sana na ashawahi andikia wasanii wa bongo mziki japo hawajamtaja. Kabla ya kusajiliwa wasafi, Mbosso alikuwa ndani ya mkubwa na wanawe. Alikuwa mmoja wa wasanii wa kikundi cha yamoto Band. Wenzake walikuwa; Aslay, Beka Flavour, Beka. Kulingana na vyombo vya habari, wasanii hawa waliachana na kila msanii kuanzisha tena upya. Kwa sasa Mbosso ni mmoja wa wasanii wa WCB na kwa sasa anafanya vizuri huku nyimbo zake zinafanya vizuri ndani ya soko la mziki.

Aslay

Aslay msanii wa Bongo

Huyu ni mwanamziki hatari. Wengi walifikiria labda angejiunga na wasafi lakini alijiamini na kufanya mziki kivyake bila kutafuta usaidizi kwa wasafi. Talanta yake ni ya hali ya juu sana na ako na mashabiki wengi wanaoamini kuwa kazi ya Aslay iko sawa.  Video zake ziko tu kawaida ila inaonekana mashabiki wake wanazipenda vile zilivyo kwani zipo na mafundisho mazuri kwa jamii yote.

Rayvanny/Vanny Boy

Rayvanny msanii wa Tanzania

Ni mmoja katika label ya wasafi. Diamond platnumz humuamini sana msanii huyu na amefanya naye cobalo nyingi sana. Kuna wakati iliwahi kusemekana kuwa alitaka kujiondoa kwa label ya wasafi ila bado anaonekana kukwama palepale. Wakati alipohojiwa na vyombo vya habari kuhusiana na kujiondoa kwake, alionekana kutokuwa na mawazo ya kuhama pale akidai diamond platnumz ndiye aliyemlea na hawezi kusajiliwa na mtu mwingine yeyote yule. Mziki wa Rayvanny unapendwa sana na watu wengi kwani pia ana uwezo mkubwa wa kuandika nyimbo zenye hisia.

Zuchu

Zuchu msanii wa bongo

Ni msanii wa kike mamake akiwa ni Khadija kopa. Kwa sasa amesajiliwa wasafi records. Ilimchukua miaka mnne kuweza kukubalika label ya wasafi. Kwa sasa msanii huyu anafanya vizuri kwa sanaa ya mziki na kwa sasa ako kwa orodha ya wasanii wa bongo wenye wanafanya vizuri. Ni hivi majuzi tu wasafi iliandaa tamasha ya kukata na shoka iliyoihudhuliwa na watu wengi sana akiwemo wema sepetu, Hamisa Mobetto na wengine wengi. Kulingana na maoni yetu, Huenda msanii huyu akakubalika kwa haraka sana barani afrika na ulimwengu mzima kwa jumla.

Venessa Mdee

Venessa Mde and Rotimi wasanii wa bongo

Ni msanii wa kike aliyetikisha ulimwengu mzima kwa miaka mingi sana. Hivi karibuni msanii huyu alitangaza kuacha mziki huku akidai kuwa usanii uko na ushetani mwingi ndio maana akaamua kuacha mziki. Venessa mde ameacha pengo kubwa kwani ni msanii tajika barani afrika. Kwa sasa ako kwenye uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa kimataifa Rotimi aliyeigiza kwa sinema ya “Power” Inayoongozwa na 50 cents.

Wasanii wa Bongo waliovuma.

Wasanii wa bongo wamekuwa wakizaliwa kila kuchao. Kama nilivyotangulia kusema, Tanzania ni nchi iliyobarikiwa sana na wasanii wa nchi hiyo wamebarikiwa na vipaji vya kuimba na kuandika pia. Hii inamanisha wasanii wa bongo wapya hujitokeza kila siku. Kama basi hauko makini, huenda watu wakakusahau kwa mda mfupi sana. Kuna wasanii wa bongo waliokuwepo miaka mingi iliyopita ila kwa sasa wengi wao wamesahaulika. Hii haimanishi talanta zao zimeshuka ila ni kwa sababu bidii ya wasanii wanaochipuka iko juu kuliko ya wale wasanii wa zamani. Ifuatayo ni orodha ya wasanii wa bongo waliokuweko na kwa sasa ni kama wamengia chini ya maji

  1. Dogman
  2. Matonya
  3. Lady Jaydee
  4. Mwana FA
  5. Ferooz
  6. Professor Jay
  7. Ray C

Kwa sasa mwangaza news itakomea hapo na tuna imani kuwa umewafahamu wasanii wa bongo japo sio wote ila tumeangazia wanaojulikana kwa mda huu na pia waliowahi kugonga vyombo vya habari na kwenye mitandao

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *