MchipukoSanaa

Willy Paul na bahati waanzisha Vita upya

Willy Paul na bahati hawakuanza Vita juzi, wawili hao wamekuwa kwenye Vita huku kila mmoja akidai ni mkali zaidi ya mwenzake.

Willy Paul amejitokeza kumjibu Bahati baada ya bahati kudai kuwa alikuwa anamwandikia Willy Paul nyimbo. Inasemekana wawili hawa walikuwa marafiki Ila kwa Sasa kumezuka tofauti Kati yao.

Bahati aliweza kuandika kwa mitandao wake kuwa anatamani zile siku wawili walikuwa marafiki huku akiongezea anatamani vile alikuwa akiandikia Willy Paul nyimbo.

Bahati pia aliweza kueka picha yake yeye na Willy Paul wakati flani wawili Hawa wakiwa kwenye Groove Awards. Hii ilikuwa mda mfupi baada ya wao kuingia kwenye Sanaa ya mziki.

“Natamani zile siku nilikuwa anamwandikia huyu kijana mdogo nyimbo, aliandika bahati

Willy Paul na bahati kwenye groove awards

 Willy Paul naye amemjibu bahati kwenye account yake ya Instagram ambapo alijirekodi video huku akiendesha Gari yake na kusema,

“Naskia mtoto wa Diana alisema alikuwa akiniandikia nyimbo… Haiwezekani… Sijui nimjibu vipi….

Baadae, Willy Paul alitoa ile post. Wawili Hawa tayari wamekili kutoka kwa nyimbo za injili na kwa Sasa wanafanya miziki ya kiulimwengu.

Soma hii pia ( pesa anazolipwa MCA Tricky )

Kuna wakati Willy Paul aliwahi kurekodi video huku akidai sauti ya bahati hairidhishi Tena. Alimuomba Diana Marua ambaye ni mkewe bahati kumsaidia mmewe badala ya wao wawili kuendelea kuharibu pesa.

“Bwana Diana utatuonyesha mambo kweli. Si uache hata Diana aimbe. Diana saidia Bwana yako we unataka ulishwe ulishwe Bwana anapoteza vocals we uko hapo unakula tu. Saidia Bwana,” he said.

Yetu itakuwa kuwaombea Willy Paul na bahati ili waweze kuelewana na kuipeleka injili mbele.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *