InternationalMaishaMchipuko

Tofauti ya maisha ya Zari Hassan na tanasha Donna ndani ya uhusiano na diamond platnumz

Zari Hassan na tanasha Donna wamewahi kuwa kwa uhusiano diaomond platnumz ila kila mmoja kwa wakati wake. Kila mmoja ana sababu zake kwa nini waliachana, na uhusiano wao ulikuwa vipi. Naye diamond platnumz ana sababu zake kwa nini aliachana na wawili hao.

Miezi imepita tangu diamond platnumz kuachana na tanasha Donna. Diamond platnumz Anajulikana zaidi kwa kuoa alafu kuacha. Hii imekuwa kawaida yake Ila wengi wanadai Kuna tofauti kuu aliyoieka Kati ya tanasha Donna na Zari Hassan.

Kwa Sasa diamond platnumz ameweza kuandikisha historian ya kuoa nchi tatu za afrika mashariki ikiwemo Kenya, Uganda na Tanzania alipozaliwa. Kwa Sasa ana familia kwa nchi nilizozitaja na kwake anaona ni Jambo kubwa ambalo lahitaji mwanaume kamili kuweza kufanya.

Kwa Sasa wengi wamekubali mwanaume huyu hawezi kaa na mwanamke mmoja kwani Tanzania nyumbani pia ana familia na Hamisa Mobetto. Wengi siku hizi washamtafutia jina mpya na wao humuita “father Abraham”. Ahadi zake zimekuwa za uongo kwa wanawake na Kama unakumbuka vizuri aliapa hatamuacha tanasha huku akitarajiwa kufunga naye pingu za maisha.

Uhusiano wake na Zari Hassan ulikaa zaidi kwani walikaa pamoja kwa miaka minne na pia kwa hiyo miaka minne wawili hao walibarikiwa kuwa na watoto wawili. Wakati huu ndipo Hamisa Mobetto naye alitokea. Inasemekana Hamisa Mobetto ndiye alikuwa chanzo Cha diamond platnumz na Zari Hassan kuachana. Baada ya wawili Hawa kuachana, naye tanasha Donna akajitia kwenye maisha ya diamond platnumz bila kujua wembe ni ule ule.

Wawili Hawa hawakukaa pamoja sana kwani baada ya mwaka mmoja, diamond platnumz na tanasha Donna walitangaza kuachana. Hii ilikuwa ni baada ya Hawa wawili kupata mtoto na pia ni baada yao kuachia nyimbo yao gere iliyokuwa imeelekezwa kwa Waliokuwa hawawatakii mema kwa uhusiano wao.

Kuachana kwa diamond platnumz na Zari Hassan kuliwafanya wawili hao kutoongeleshana kwa mda kwani Kulingana na Zari Hassan, aliumizwa sana na diamond platnumz sana sana aliposikia ana uhusiano na Hamisa Mobetto. Zari Hassan aliamua kurudi kwao na kuapa kutorudiana na diamond platnumz huku akiamua kulea watoto peke yake.

Zari Hassan na tanasha Donna kwenye ubora wao

Sababu ya Zari Hassan kuachana na diamond platnumz

Zari Hassan alisikika akisema kuwa amekuwa akivumilia diamond kwani amemshika Mara nyingi na wanawake tofauti. Siku ya wapendanao mwaka wa 2018, Zari Hassan alionekana kuchoka kabisa na uhusiano wake na diamond platnumz na kuamua kumuacha baada ya kumshika na mwanamke.

Sababu ya tanasha Donna kuachana na diamond platnumz

Haijajulikana vizuri ni kwa Nini tanasha Donna na diamond platnumz waliachana Ila Kuna fununu kwamba diamond alikuwa na mchepuko. Wawili Hawa walikataa kabisa kuongelea tukio Hilo kwa vyombo vya habari. Kwenye wasafi radio, diamond alisikika akisema hawezi ongea chochote kwani mwenzake tanasha Donna hajaongea chochote. Aliongezea kusema Kuna vitu tu hawakuelewana ndio maana kila mtu aliamua kwenda kivyake Ila hakuelezea kwa undani kabisa.

Wakati tanasha Donna alipoachana na diamond platnumz, mafans walijua kwa haraka sana kwani tanasha Ali unfollow diamond na kufuta picha zake na za familia yake na hata kutoa jina la diamond platnumz kwenye profile ya mwanao. Zari Hassan na tanasha Donna wanaoneka kupitia maisha magumu ila kila mmoja aliona avumilie kwa mda japo maji yalizidi unga.

Kulingana na utafiti wetu, zari Hassan ndiye alikuwa kipenzi Cha mama diamond. Habari zingine zilidai kuwa, mamake diamond ndiye alikuwa chanzo kikuu Cha tanasha Donna na diamond platnumz kuachana. Ili kuweze kuwa na uhusiano na diamond platnumz, lazima mamake diamond akupende mwanzo na Kama hakupendi, Basi hauna lako.

 Zari Hassan na Mama Diamond ( Mama Dangote) | Zari Hassan na tanasha Donna

Baada ya diamond kuachana na Zari Hassan, wawili hao waliongea sana ndani ya vyombo vya habari kila mmoja akilaumu mwenzake kwa mchepuko na hakuna aliyetaka kuonekana Kama chanzo Cha wao kuachana. Zari Hassan pia aliongezea kuwa diamond hashughulikii watoto wake. Hii ilikuwa tofauti Kati ya diamond platnumz na tanasha Donna kwani wote waliamua kukaa kimya kwa vyombo vya habari. Diamond platinumz amejitokeza juzi na kusema washaongea na Zari Hassan na wamekubaliana jinsi watakavyolea watoto wao.

Zari Hassan na watoto wake

Juzi diamond platnumz amesema kuwa yeye alikuwa tayari kumuoa tanasha Donna ni vile tu vitu havikuenda alivyotarajia akiongezea kuwa hajawahi enda nje ama kuwa na mwanamke mwingine wakati huu alipokuwa na tanasha Donna. Ukiangalia upande wa Zari Hassan, diamond platnumz hakuwahi kutamka kumuoa Zari Hassan japo wawili Hawa walipata watoto wawili pamoja. Usisahau kueka notification On kwa kugonga kengele ilioko pembeni ili kila siku uweze kuwa wa kwanza kupata habari zetu kamilifu

Soma hii pia ( Tazama tanasha alivyoiaga familia ya Diamond Platnumz)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *