Mchipuko

Zari Hassan apata afueni tazama alichokifanya diamond platnumz

Zari Hassan aliyekuwa mke wa diamond platnumz ana furaha isiyo na kipimo. Hii ni baada ya diamond kuregelea maisha ya watoto wake. Kwa miaka miwili iliyopita, Diamond platnumz hakuwa na mchango wowote kwa watoto wake aliowazaa na zari Hassan.

Wawili hawa waliacha siku ya wapendao “valentine day” mwaka wa 2018. Kutoka siku hiyo diamond platnumz alijitoa kabisa na alikuwa hatoi hata peni moja ya kusaidia malezi ya watoto wao. Juzi mambo yamegeuka na wawili hao wanashirikiana kuwalea watoto wao.

“Baada ya miaka miwili, diamond platnumz ambaye ni baba wa watoto wangu ameelewa makosa yake na amekubali kuwasaidia watoto wetu. Nimefurahi sana kwa Hilo na itakuwa sio haki nisipotoa shukrani zangu kwake..” alisema zari Hassan..

Aliendelea na kusema kuwa sio eti ajipendekeza ila malezi ya watoto wake ni mhimu baba yao akiwa karibu

“Kwa vile amerudi sasa mnasema najipendekeza. Sio hivyo kabisa. Najua kuna watoto huko nje wanarandaranda mitaani maana mama zao wamewanyima malezi ya baba zao. Baba watoto ni mhimu sana katika malezi ya watoto…”

Aliongezea na kusema

“Mnaongea sana kila siku matusi mwaka mzima mkijibiwa moja tu mnaharisha wiki nzima….shenzy type…tulieni dose nyengine yaja…”

Diamond platnumz alipoachana na zari alimuoa tanasha Donna ambaye ni mkenya. Baada ya kuzaa mtoto mmoja waliachana na tanasha Donna akarudi Kenya. Kwa sasa wawili hawa hawamo kwa uhusiano

Soma hii pia ( je, diamond platnumz na zari wanarudiana?)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *