MchipukoMaisha

Director Kenny atimuliwa na Diamond Platnumz

Kama umekuwa mtu wa kufuatilia mitandao basi utakuwa unamfahamu director Kenny. Gwiji huyu ndiye alikuwa akiongoza karibu video zote za wasafi.

Kenny amekuwa kama zaidi ya rafiki wa diamond platnumz na wamekuwa wakiandamana kwa kila shughuli hata za kifamilia. Director Kenny aliletwa ndani ya wasafi na harmonize baada ya kumtoa kwa hanscana.

Katika Instagram yake, Kenny alifuta maelezo yake kuhusu kufanya Kazi na zoom extra inayomilikiwa na Diamond Platnumz. Kulingana na habari za hapa na pale, vyombo alivyokuwa akizitumia director Kenny zimekabidhiwa hanscana.

director Kenny Instagram

Kama umekuwa ukifanya utafiti wako utakuwa umegundua kwamba video nyingi za wasafi zinazoachiliwa kwa sasa zimeongozwa na hanscana. Hizi video ni kama vile nyumba Ndogo yake Zuchu, sweet ya Rayvanny ft. Guchi na Iyo yake Diamond platnumz. Kamata aliyoachia diamond platnumz iliongozwa na Kenny Ila Kulingana na utafiti wetu, video hii ilifanyika mwaka Jana.

Kwa sasa tunangojea tuone hatua atakayoichukua director Kenny. Wengi wanasema huenda akamfuata harmonize ambaye alimleta wasafi ama labda wataelewana na Diamond platnumz na huenda akarudi wasafi. Hapa mwangaza news letu ni jicho tu na habari zaidi zikipatikana kuwajulisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *