Historia

Historia Ya Mandonga Mtu Kazi

Historia Ya Mandonga ina mengi sana ila tutaongelea bingwa huyu kwa kifupi.  Ni bondia kuokea nchi ya Tanzania anayekulikana kwa jina maarufu kama mtu kazi. Kulingana na yeye, hakuna anaweyemuweza katika mchezo wa bondia ndani ya afrika mashariki

Juzi amekuwa nchini Kenya na aliweza kumshinda mpizani wake kwa jina wamalwa. Japo mkenya alionekana kumzidia raundi ya kwanza, Mandonga alijitahidi na kuwa mshindi baada ya raundi ya tano. Zidi kutegea hapa upate mengi kuhusiana na historia ya mandonga.

Umri wa Mandonga Mtu kazi

mandonga mtu kazi age

Ikiwa ni mwaka wa 2023 napoiandika historia ya bingwa huyu, Mandonga ako na umri wa miaka 44. Majina yake kamili ni Karim H Said. Alizaliwa nchini Tanzania sehemu inayojulikana kama Mkundi. Alianza mchezo wa bondia mwaka wa 2015 na mpaka Leo anaendelea na huu mchezo anaoupenda zaidi.

Karim Mandonga hupenda kuongea sana na labda mdomo wake humsaidia kufaulu kwa kazi zake. Wasanii kadhaa kutoka nchi ya Tanzania wamemfanyia nyimbo za kumsifu akiwemo bella 9 aliyemfanyia nyimbo kwa jina Mandonga.

Pigano Mandonga na wamalwa nchini Kenya

Wengi wamemjua bondia huyu kupitia hili pigano. Mandonga aliweza kujaza ukumbi wa KICC nchini Kenya. Kukingana na utafiti wetu, aliyekuwa amepanga shindano hilo aliingiza mamilioni ya pesa. Mandonga alimshinda mpizani wake kwenye raundi ya tano japo mwanzoni alikuwa amelemewa ila mwishowe alijitahidi na kuwa mshindi

Pigano Hilo la mandonga na wamalwa limemsaidia sana Mandonga kwani tayari ashazawadiwa magari mawili. Kulingana na yeye, Gari moja ataachia mkewe na watoto naye atabakia na moja aina ya Subaru.

Majibizano ya Mandonga na salaam Sk meneja wa diamond platnumz

Baada ya kuwa mshindi nchini Kenya, salaam Sk alimpongeza ila pia alikuwa na ushauri kwake. Salaam Sk alimshauri Mandonga awache kuwatajirisha matajiri na achukulie kazi yake kama biashara asije kujuta baadae. Mandonga naye akajibu kuwa kazi anayoifanya ni yake mwenyewe na anaelewa faida zake mwenyewe

Ni hayo tu kwa sasa kuhusiana na historia ya mandonga. Zidi kufuatilia taarifa zetu za mwangaza news kwa mengi zaidi.

Pia soma historia ya Historia ya Kajala Masanja

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *