HistoriaMaisha

Historia ya Rayvanny : Je Rayvanny ana miaka mingapi

Wengi wanamjua kama Rayvanny ila majina yake Kamili ni Raymond Shaban Mwakyusa. Historia ya Rayvanny ni ya kipekee na wengi wamekuwa wakiulizia maisha yake vile yalikuwa hapo awali.

Ni msanii kutoka nchi ya Tanzania na ana uwezo wa kuimba pamoja kuandika nyimbo. Japo sasa ako na label yake inayojulikana kama Next level music, bado ako chini ya WCB iliyochini ya diamond platnumz.

picha ya Rayvanny na diamond platnumz

Kwa sasa anajivunia kuwa na label yake ya next level music kama C.E.O. Nyimbo yake ya kwanza aliyoifanya na kumpa umarufu mkubwa inajulikana kama “Kwetu” nyimbo hii ilirekodiwa mwaka wa 2016 na ndio ilimfungulia njia kama mwanamziki. Kabla ya hapo alikuwa bado anarekodi japo nyimbo alizokuwa amerekodi hapo awali hazikumpa umarufu.

Alijiunga Label ya WCB mwaka wa 2015 ila akiachia nyimbo yake ya kwanza mwaka uliyofuatia 2016. Hii Ina maana alichukua mda wake kuisoma game ya mziki na pia kupata mafunzo kwa mwalimu wake ambaye ni diamond platnumz.

Rayvanny ni msanii tunaweza sema alikuwa na bahati sana kwani mwaka wa 2017 alichaguliwa msanii wa kwanza Tanzania kuwania tuzo za BET kama mmoja wa “The bet viewers choice na Best new international Act”

Rayvanny hakuwabwaga mashabiki wake kwani alinyakua tuzo hiyo na kuwa msanii wa pili afrika mashariki kupata tuzo la BET. Msanii wa kwanza alikuwa Eddy Kenzo aliyeshinda tuzo hiyo mwaka wa 2015.

Mwaka wa 2020 Rayvanny alibahatika tena kwani alikuwa mmoja wa kuwania tuzo za Grammy awards. Hii ni baada ya kuachia Ep yake ya dubbed flowers.

Je, Rayvanny ana miaka mingapi?

Rayvanny alizaliwa mnamo august tarehe 22 mwaka wa 1993. Alizaliwa sehemu inayojulikana kama Mbeya nchini Tanzania. Wazazi wake hawakuwa na uwezo mkubwa kifedha ila waliweza kumlea Rayvanny kwa tabu mpaka akakua.

Wazazi wake wamekuwa wakimpa sapoti toka akiwa mdogo mpaka sasa. Rayvanny anaye ndugu yake anayejulikana kama Shadrack ambaye hivi majuzi amehitimu ndani ya Ardhi university iliyoko Tanzania.

Alianza kupenda mziki akiwa shule ya msingi na alipokuwa shule ya upili, Rayvanny alishinda mashindano ya kufyoka ama ukipenda rap battle iliyoandaliwa na Seringeti. Mwaka wa 2011, Rayvanny alipata ushindi katika kiwango Cha kimataifa ( national competition mjini Dar es salaam Tanzania.

Rayvanny alianza mziki mwaka wa 2012 baada ya kujiunga na kikundi cha Tip Top connection kilichokuwa chini ya Babu tale. Ashawahi kuwa back up singer wa Madee Ali na pia yamoto band. Hapo ndipo safari yake ya mziki ilipoanzia na akaanza kufanya Kazi kama yeye

Baada ya kufanya Kazi kadhaa ndani ya Tiptop, diamond platnumz aliona uwezo wake na akaamua kumchukua ili afanye Kazi na yeye kwani aliona uwezo mkubwa kwake. Hii ilikuwa mwaka wa 2015 ambapo kilichofuatia ni nyimbo ya kwetu na kutoka hiyo siku, Rayvanny amekuwa akifanya bidii sana kwani hajawahi Rudi nyuma.

Familia na uhusiano wa Rayvanny

Rayvanny alikuwa kwenye uhusiano na Fayhima ama ukipenda Fayvanny ambaye ni mwanamitindo. Wako na mtoto pamoja anayejulikana kama Jaydan vanny.

Rayvanny na fayhma

Kwa sasa wanamlea wote wawili japo hawako pamoja na kwa sasa anasemekana kuwa na uhusiano na Paula Kajala ambaye ni mwanawe Frida kajala aliyekuwa mpenzi wa harmonize

picha ya Rayvanny na Paula Kajala

Tuzo alizoshinda Rayvanny

Mwaka wa 2016, Rayvanny alichaguliwa kuwania tuzo za MTV afrika kwenye kitengo Cha breakthrough Act japo hakushinda. Mwaka wa 2017 alishinda tuzo ya Best new international Act ndani ya BET Awards

Mwaka huo huo, Rayvanny alichaguliwa kuwania tuzo za the best newcomer ndani ya African music magazine awards ila hakushinda. Mwaka wa 2019, Rayvanny aliibuka mshindi kama best male artists kwenye tuzo za start awards ndani ya Johannesburg nchini south Africa. Hakukomea hapo kwani mwaka huohuo alipata tuzo ya Annual African entertainment awards U.S.A kama best male artiste in East, south and north Africa.

Mwaka wa 2020 alijaribu pia kuwania tuzo za Grammy awards kupitia Ep yake ya dubbed flowers. Mwaka huohuo alipata tuzo ya Best male African entertainment awards USA tena.

Mwaka wa 2017, Rayvanny alikuwa mmoja wa wasanii waliyochagulia ndani ya coke studio. Alipata nafasi ya kufanya Kazi na Dji tafinha. Wasanii wengine waliofanya kazi nao ndani ya coke studio ni mwanamziki wa marekani, Jason Derulo, Dela na Bebe cool na nyimbo waliyoifanya ilikuwa inajulikana kama push up on it.

Mwaka wa 2019, Rayvanny alipata nafasi tena ya kuingia ndani ya coke studio na safari hii alifanya Kazi na Naiboi pamoja na laizer classic.

Ugomvi wa Rayvanny na harmonize

Mwaka wa 2021 vita baina ya harmonize na Rayvanny zilizuka kwani harmonize alikuwa akilaumu Rayvanny kwa kumtongoza mtoto wa kajala ambaye ni Paula. Kulingana na harmonize, Paula alikuwa mdogo sana na Rayvanny angemharibia maisha yake

picha za Rayvanny harmonize

Naye Rayvanny pia alitoa malalamishi yake na kusema harmonize pia humtumia Paula picha zake za uchi. Kwa sasa Paula ni mpenzi wa Rayvanny na inasemekana yeye ndiye anayesimamia masomo ya binti huyu

YouTube Channel ya Rayvanny

Rayvanny alijiunga na YouTube March 17 mwaka wa 2016. Kwa sasa idadi iliyotazama kazi yake ni zaidi ya milioni mia sita. Mwaka wa 2019 alipata tuzo ya YouTube gold ambayo hupatikana ukipata subscribers milioni moja.

Soma hii pia : historia ya hamisa mobetto

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *