MaishaHistoria

Historia ya Wema Sepetu

Historia ya Wema Sepetu ni yakuigwa na ni tofauti sana. Kumbuka mrembo huyu ndiye aliyechangia pakubwa sana kwa kujulikana kwa diamond platnumz. Kwa majina kamili Anajulikana kama Wema Sepetu

Wema Sepetu ni mwanamke mrembo aliyeweza kujulikana na kugonga vichwa vya habari tangu mwaka wa 2006 wakati alipochaguliwa kama miss word Tanzania 2006. Bado yupo na hajapotea na anajihusisha na biashara zake mpaka wa Leo

Wema Sepetu ana miaka mingapi

Wema Sepetu alizaliwa nchini Tanzania mwaka wa 1988 hii Ina maana kwamba mwaka wa 2022, Wema Sepetu ana miaka 34.

Historia ya Wema Sepetu

Uhusiano wake na diamond platnumz ulimfanya Wema Sepetu kujulikana hata nchi jirani. Kumbuka alikuwa mpenzi wake diamond platnumz. Japo uhusiano wake na diamond hakuwa wa mda mrefu kwani baadae diamond alimuacha na kunzisha uhusiano mpya na Zari Hassan. Wema Sepetu alizidi kujulikana zaidi kupitia Diamond platnumz.

Kumbuka wawili hawa walijuana kabla diamond platnumz hajatoka kabisa kimziki. Hii Ina maana kwamba, kutoka kwa diamond kimziki kulikuwa na mchango wake Wema Sepetu

Picha za Wema Sepetu

Masomo ya Wema Sepetu

Masoma yake Wema Sepetu yalianza mjini Dar es salaam Tanzania na baadae akasafiri nchi ya Malaysia kwa masomo zaidi. Huko Malaysia, Wema Sepetu alihitimu katika masomo ya biashara.

Hata kama alisomea biashara, Wema Sepetu aligundua kwamba biashara haikuwa “passion” ama lengo lake kwani filamu ndio ilikuwa “passion” yake. Aliaachana na maswala ya biashara na kufuata ndoto zake za kuwa muigizaji. Kwa bahati nzuri filamu ilizidi kumpa jina afrika nzima.

Kwenye filamu alikutana naye Steven Kanumba ambaye ni marehemu. Kanumba alikuwa Gwiji kwenye filamu na alichangia pakubwa sana katika kukuza talanta ya Wema Sepetu.

Sinema ya kwanza aliyoifanya na Steven Kanumba ilijulikana kama “A Point of return”. Movie hii ilipata utazamaji mkubwa sana na Wema Sepetu akazidi kuwa maarufu. Movie nyengine alioigiza ni “White maria” ambayo pia ilipata utazamaji zaidi. Wema Sepetu aliwahi kuwa kwenye uhusiano na Steven Kanumba.

wema Sepetu photos

Baada ya kuigiza kwa movie kadhaa, Wema Sepetu alihitimu kama mtayarishaji wa filamu na kuanza kutayarisha movie zake. Movie yake ya kwanza aliyoifanya wakati akiwa na uhusiano na diamond platnumz haikuweza kuwachiwa kwani alikosa mtu mzuri wa kuinunua au kusambaza

Hakufa moyo aliendelea kufanya Kazi na wanafilamu tofauti akiwemo Van Vicker ambaye anatokea Nchini Ghana. Wema ameigiza kwa filamu zaidi ya ishirini na kusema kweli amepiga hatua kubwa sana kwenye soko la filamu kwani ana kampuni yake pia inayojulikana kama Endless Fame Production.

Kwenye historia ya Wema Sepetu, hatuwezi sahau tuzo zenye amepata akiwa ndani ya filamu. Tuzo hizi ni kama vile Sinema Zetu international film ambapo alipata tuzo kama muigizaji bora wa kike mwaka wa 2018. Hii ni baada ya kuigiza kwenye sinema ya ” “heaven sent”. Pia alipata Tuzo za Nzumari kama muigizaji wa kike bora mwaka wa 2015.

Wema Sepetu ana wafuasi wengi kwenye mitandao kama vile Instagram. Hii humuwezesha kufanya biashara za matangazo na kampuni nyingi Nchini Tanzania.

Utajiri wa Wema Sepetu

Ni mwanamke anayesemekana kuwa tajiri sana. Ana nyumba za kifahari na magari aina tofauti. Hupata pesa zake kupitia filamu na pia ubalozi katika bidhaa tofauti. Kwa sasa utajiri wa Wema Sepetu unakisiwa kuwa milioni $2.

Tutakomea hapo Kwa Leo kuhusiana na historia ya Wema Sepetu. Zidi kufuatilia habari zetu hapa mwangaza ili uweze kufahamu mengi zaidi.

Soma hii pia: Historia ya Paula masanja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *