MaishaHistoria

Historia ya Paula Kajala

Japo bado mdogo, historia ya Paula Kajala ipo na vitu mingi sana vya kuongelewa. Kwa mda amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa mambo kadhaa ikiwemo uhusiano wake na Rayvanny.

Paula kajala ni mwanamitindo na majina kamili Anajulikana kama Paula Paul majani. Ni mtoto wa mtayarishaji wa mziki p fank majani. Mamake pia ni maarufu kwani amekuwa akiigiza kwa filamu za bongo kwa mda mrefu. Mamake Paula Anajulikana kama kajala masanja.

Paula alijulikana zaidi wakati mamake alikuwa mpenzi wake harmonize. Kuna mda pia ilisemekana kwamba, Paula na harmonize pia walikuwa na uhusiano wa Siri bila mamake kajala kujua.

Umri wa Paula masanja

Kwa sasa ( mwaka wa 2021) Paula Kajala ana miaka kumi na tisa. Alizaliwa mwaka wa 2002 na ndiye mtoto wa kike pekee wa muigizaji Gwiji kutoka Tanzania, Frida Kajala masanja na mtayarishaji wa mziki Paul matthysse ambaye kwa jina la utani Anajulikana kama P Funk Majani

Masomo ya Paula

Baada ya kusambaa kwa video yake na Rayvanny wakiwa kwenye matukio ya mapenzi, ndipo ilipojulikana wazi kwamba Paula bado ni mtoto na anasoma. Wakati huo alikuwa kidato cha tano na alikuwa bado hajafikisha miaka kumi na tisa.

Ndoto za Paula zilikuwa ni kuendelea na masomo ya theater na fashion design ambapo kwa sasa yupo nje ya nchi na anaendelea na masomo. Pia inasemekana Rayvanny ndiye anaghalamikia ada ya shule.

Uhusiano wa Rayvanny na Paula kajala

Miezi kadhaa iliyopita, kulitokea video ya Rayvanny na Paula wakionekana kuwa kwenye hali ya mahaba. Video hii ilisambaa sana kwa mitandao. Video hii inasemekana kurekodiwa na Hamisa Mobetto ambaye alikana kurekodi hizo video.

Paula masanja

Kajala masanja alimkasirikia sana Hamisa Mobetto huku akidai anamfundisha mwanawe tabia mbaya kwa kumulewesha. Hamisa alijitetea na kusema yeye na Paula walipata chakula Cha mchana alafu wakaachana na hakuna wakati walikutana na Rayvanny.

mamake Paula Kajala

Paula aliendelea kugonga vyombo vya habari baada ya Rayvanny kuachia chat na video za harmonize na Paula. Video hizo zilionyesha sehemu nyeti za harmonize zinazosemekana alikuwa akimtumia Paula kupitia chati zao.

Wakati huohuo harmonize alikuwa kwenye uhusiano na mamake Paula na hii huenda ikawa ndio sababu Rayvanny aliamua kuachia hizo video. Kumbuka video ya Rayvanny na Paula ilipotokea waki kiss, harmonize alikuwa wa kwanza kumkashifu Rayvanny akidai kwamba Rayvanny anafanya mapenzi na mtoto wa umri wa miaka kumi na nane na hairuhusiwi.

Paula harmonize Kajala masanja

Kwenye Instagram page yake, Rayvanny alisema alishangazwa sana na harmonize kwa kile alichokifanya na yeye ndiye alikuwa wa kwanza kumkosoa Rayvanny kwa video yake na Paula. Rayvanny aliongeza kwamba haamini tendo la harmonize kumtaka Paula wakati tayari alikuwa na uhusiano na mamake Paula.

“Unataka kua na mama na mtoto…na Unatuma hadi utupu wako bila hata kuogopa,” Rayvanny aliandika kwa Instagram page yake.

Utajiri wa Paul Kajala

Kwa sasa itakuwa vigumu kutaja utajiri wa Paul Kajala kwani ndio ameanza kujulikana na bado mdogo. Pia nyumba ama magari zake hatuwezi kuzifahamu kwa sasa. Huenda akawa ana utajiri mkubwa tukizingatia mamake amekuwa kwa filamu kwa miaka mingi.

Wakati tutapata habari kuhusiana na Mali ya Paula Kajala, tutawajulisha hapahapa mwangaza news. Hiyo ndiyo historia ya Paula Kajala kwa sasa. Zidi kufuatilia habari zetu hapa mwangaza news.

Soma hii pia :

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *