MchipukoHistoriaMaishaSanaa

Historia ya Zuchu

Historia ya Zuchu

Japo wengi wanamfuatilia msanii huyu wa kike kutoka label ya WCB, ni wachache wanaojua historia ya Zuchu. Kwa mda mfupi, msanii huyu amefaulu kimziki na kwa sasa yupo vinywani mwa watu wengi ulimwengu mzima.

Maisha ya Zuchu

historia ya Zuchu

Kwa majina kamili Anajulikana kama Zuhura othman soud. Alizaliwa tarehe ishirini na mbili  mwaka wa 1993

Zuchu alizaliwa Zanzibar sehemu inayojulikana kama kwahani. Alizaliwa katika hospitali almaarufu kwa jina mnazi mmoja iliyoko zanzibar. Zuchu amesomea zanzibar kuanzia chekechekea mpaka akamaliza shule ya upili.

Baada ya kumaliza shule ya upili, zuchu alisafiri hadi india kwa masomo zaidi. Huko ndipo alijiunga na chuo kikuu huku akijiingiza kwa masomo ya uchumi na biashara. Kwenye chuo kikuu alisomea masomo kama vile commerce, economy na computer. Science. Alipata shahada ya advance diploma ndipo akarudi nyumbani zanzibar. Akiwa mdogo, Zuchu alitaka kuwa mwanasheria ila mamake hakupenda kwani Kazi hiyo aliichukulia kama Kazi ya laana tupu. Hii ni kwa sababu kuna wakati wanasheria wanatetea watu hata kama wamebaka.

Zuchu hakuanza kupenda mziki juzi kwani hata alipopelekwa shule, wazazi wake walimuomba mwalimu wake asije akamuruhusu ajiunge na kwaya ama vikundi vya mziki wakiogopa asingesoma kwa vile alipenda kuimba kuanzia akiwa hata hajajiunga na chekechekea.

Wakati akiwa mdogo, hakuweza kupata mda na mamake Khadija kopa kwani kama ujuavyo, mamake ni mwanamziki hivyo Mara nyingi alikuwa kazini mjini. Zuchu ametoka kwenye familia ya wanamziki akiwemo Babake, kakake omar kopa na mamake Khadija kopa.

Kuwa mtoto wa Khadija kopa kulitatiza sana maisha ya Zuchu kwani wengi shuleni walidhania angekuwa shangingi. Hii ni kwa maana mamake alikuwa msanii wa mziki wa taarab na uswahilini waliuchukulia mziki aina ya taarab kama mziki wa waswahili.

Vile mamake zuchu alikuwa Mara nyingi hapatikani nyumbani, kakake zuchu omar kopa ndiye alikuwa kama mlezi wa zuchu. Wawili Hawa walikuwa na ukaribu sana na walipendana sana. Siku omar kopa alipoaga dunia, ilibidi zuchu asijulishwe mpaka wakati Omar kopa amezikwa ndipo zuchu akajulishwa.

Kifo Cha kakake kilimtatiza sana mpaka wa leo kwani zuchu hawezi skiza nyimbo za kakake. Akihojiwa kwenye wasafi Tv, zuchu alisema kuwa hata akipatana na mtu akiskiza nyimbo za omar kopa humwambia azime maana huwa zamkumbusha mbali. Kifo Cha kakake kilitokea akiwa darasa la tano na mpaka wa leo hajui kaburi lake lipo wapi.

Babake waliachana na mamake akiwa bado mdogo hivyo hakuweza kuyafurahia maisha ya mzazi wa kike na wa kiume. Babake zuchu alikuwa polisi hivyo pia kuonana ilikuwa bahati. Wakati zuchu akiwa mdogo alikuwa yuapenda kumpelekea Babake zawadi kwenye kambi ya polisi.

“Nakumbuka kuna mda nilimtamani babangu mpaka nikamuandikia barua ili anipe pesa za kusherekea eid…. babangu alipopata barua yangu alisafiri akaja hadi nyumbani na kunizawadi shilingi Elfu ishirini za tanzania.. kumbuka wakati huo zilikuwa na dhamana……”

Wakati zuchu yupo masomo india hawakuwa wanawasiliana sana na Babake. Hata kama Zuchu alikuwa na mamba za Babake za simu, hakupiga simu kwani alitaka kujua Kama Babake angemtafuta. Kulingana na Zuchu, Babake hakuwahi kumpigia simu ndipo akaamua kumtumia arafa na kumsalimia huku akijitambulisha kama mtoto wake… Cha maajabu, Babake alimjibu “sawa”. Hii ilimfanya zuchu kukasirika mpaka akaamua kutomuongelesha Babake kabisa.

Mwaka jana wakati wa kampeni za magufuli ndipo alipopokea ripoti kutoka kwa mamake kuwa Babake hajihisi vizuri. Iliwalazimu yeye na mamake kusafiri hadi kwa Babake. Babake alipomuona zuchu alitokwa na machozi huku akimkumbatia kwa hisia. Zuchu hata hakutaka kumuuliza Babake kwa nini huwa amempuuza ilibidi tu akubali matokeo.

Kulingana na yeye, kufanikiwa kimziki ni baraka za mwenyezi Mungu na bidii yake. Anashukuru la label ya wasafi na mamake mzazi kwa kumsukuma kwenye media.

Safari ya Zuchu ya mziki

zuchu husband

Je, wajua ilikuwa aje mpaka akafanya colabo na diamond platnumz?
Kulingana na Zuchu, cheche instrumental ilikuwa yake diamond platnumz. Akiwa studio kama kawaida yake, producer alimuekea zuchu hiyo beat na Zuchu akaipenda sana. Akakata producer amuachie ila producer akamwambia ni ya diamond na kama anaitaka basi itabidi akaongee na diamond mwenyewe.

Baada ya Zuchu kumuomba diamond ile beat, aliachiwa lakini kwa masharti. Arekodi nyimbo kama itakuwa nzuri ataachiwa ikiwa mbaya amregeshee diamond Platnumz beat yake. Hii ilikuwa kibarua kwake lakini alijitahidi sana.

Alipoeka verse 1 alimtafuta Rayvann ili aweze kusikiza aseme kama nyimbo ni nzuri ama mbaya. Rayvann aliipenda sana hiyo nyimbo. Ni siku moja wakiwa kwa gari pamoja na Diamond, Rayvann alimwambia zuchu aieke ile nyimbo boss wake diamond asikize. Diamond aliipenda sana. Zuchu alimuomba diamond kueka verse ambapo diamond alimtaka zuchu kurekodi nyimbo yote akiipenda ataweka verse.

Wakati huohuo kulikuwa na beat ya litawachoma na pia wawili hawa walirekodi pamoja. Kulingana na Zuchu, hizi nyimbo zilipotoka, walishindwa hata kuchagua watachilia ipi mpaka wakaamua kuachia zote. Cheche ilionekana kupendwa sana kwani inachezeka ila litawachoma ilipoachiliwa, ilipata mapokezi mazuri zaidi.

Cheche na litawachoma zilipendwa na ziliweza ku trend karibia mwezi zikiwa namba moja na namba mbili. Ndani ya label, wengi walipenda cheche na kila mtu alitaka diamond platnumz kuweka verse.

Ukaribu wa Zuchu na diamond platnumz

diamond platnumz zuchu

Kuna wengi walifikiria labda kuna kitu kinaendelea Kati ya Zuchu na diamond ila Kulingana na Zuchu yeye na boss wake wanaheshimiana sana. Sio diamond tu ila ma boss wote wa WCB anawaogopa na anawaheshimu sana.
Zuchu alisema kwamba kuna vitu vyake binafsi huwa hata hawezi kuongea na ma boss wake kwani anawaogopa.

Zuchu kushindanishwa na Nandy hakumsaidii katika maisha yake na sio Nandy tu hata msanii mwingine yeyote yule. Yeye anafanya Kazi yake ya mziki na kuhakikisha nyimbo anazofanya zinampatia mapato kwani kushindanishwa hakuleti hela kwake.

Mwaka jana Zuchu alikuwa nominated kama msanii chipukizi Afrima. Aliweza kushinda tuzo na hii ilimfurahisha sana. Kulingana na yeye, nomination peke yake ilimfurahisha na alipotangazwa kama mshindi, hakuamini ila alifurahi sana.

Kwa sasa zuchu amepata umaarufu ulimwengu mzima. Ni juzi tu gazeti la spain lilimfanisha msanii huyu na beyonce na kusema Zuchu ni beyonce wa afrika. Habari kama hizi zina mpea moyo zaidi zuchu kwani anaiyona bidii yake.

Zuchu amefanya colabo na wasanii wengi ila kwake, my number one yake na Rayvann ndio anayoipenda zaidi. Zuchu kwa sasa hayupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na yeyote na kwa wale walifikiria anatoka na wasanii wenzake basi ajue sivyo.

Rayvann zuchu number one

“Sijawahi kulala na mtu yeyote kwa industry awe ni producer, msanii ama promoter…..
Ikiwa una subiria kitu kwenye maisha yako, usikae tu.. fanya bidii ili wakati ukifika uwe uko tayari… Kumbuka Mda sahihi ni mda wa mungu asikundanganye mtu ….”

Zidi kutegea mwangazanews kwa mengi zaidi

Soma hizi pia 👇

Soma hii pia ( majina kamili ya waigizaji wa selina maisha magic)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *