MaishaMchipuko

Jalang’o akanusha madai ya Omosh kuwa hakupokea milioni moja

Mtangazaji mashuhuri jalang’o amekanusha madai ya aliyekuwa muigizaji wa Tahadi high Omosh. Omosh alidai alipokea pesa ambazo hazikuzidi million moja kutoka kwa mchango wa wakenya.

Omosh jalang'o

Alitangaza haya wakati alikuwa akifanya mahojiano ndani ya televiseni ambapo alitaka msaada zaidi kutoka kwa wakenya. Ni miezi nne tu imepita tangu achangiwe na tayari inaonekana pesa yote imeisha.

Omosh ambaye jina yake kamili ni Peter Kinuthia alikuwa mashuhuri ndani ya kipindi Cha Tahidi high kilichokuwa kikipeperusha kila siku ya juma nne ndani ya citizen Tv. Tamthilia ya Tahidi high  ilikuwa ikiangazia maisha ya wanafunzi shuleni.

Omosh Tahidi high

Katika tamthilia hii ya Tahidi high, Omosh alikuwa akiigiza kama mlinzi na alikuwa kipenzi Cha watu. Baada ya kuonyeshwa miaka kumi na nne, Tahidi high ilisimamishwa mwaka wa 2020 na hapo ndipo Omosh alijikuta hana Kazi.

Omosh wives

Mnamo tarehe 12 February mwaka wa 2021, kituo kimoja Cha habari kilimhoji Omosh. Huko akitokwa na Machozi, Omosh alisema anadaiwa laki na hamsini. Wakenya walijukusanya kwa mitandao wakiongozwa na mtangazaji Felix Odiwour a.k.a jalang’o na kuahidi kunachangia Omosh shilingi milioni moja.

Kampuni ya Zero Hero properties limited iliingilia Kati na kumpatia Omosh ploti yenye gharama ya laki tano. Juzi Omosh akihojiwa alikanusha kwamba alipata milioni na hapo ndipo jalang’o alijitokeza kutetea wakenya waliomchangia.

” Watu wengine hawawezi jifunza, nawahakishia kwamba Omosh alipokea zaidi ya milioni moja kupitia show yangu,” jalang’o aliandika.. alipata pesa taslimu laki saba na Kuna watu walimtumia moja kwa moja kupitia kwa simu yake..”

photos of Omosh house

Jalang’o pia alitaja kampuni iliyojitolea kumjengea Omosh nyumba huku akiongezea kwamba mwanasiasa kutoka Nairobi Alinur Mohammed alimpa chakula iliyogharimu Elfu sitini na akampatia laki moja pesa tasilimu.

alinur Mohammed Omosh
alinur Mohammed na Omosh

Mheshimiwa alinur pia alishangazwa na tukio la Omosh kutaka kuchangiwa tena na kusema kuwa ameshangazwa kwani alijitolea kumsaidia kumbe baadae Omosh hakuona bidii yake.

Soma hii pia ; historia ya Bahati

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *