Jinsi ya kufungua youtube channel ya kulipwa
Kuna watu wengi sana wamekuwa wakiulizia Jinsi ya kufungua youtube channel ya kulipwa. Hii ni rahisi sana na kila mtu anaweza kuwa na channel yake ya youtube. Unachotakiwa kufanya ni kufuata taratibu zifuatazo.
Youtube channel ni nini?
Hii ni tovuti inayotumika ulimwengu mzima kuhifadhi video na pia inampa mtu uwezo wa kutazama video zilizoko kwenye tovuti hii. Kwa sasa youtube iko miongoni ya tovuti zinazoongoza kwenye mitandao huku google ikishikilia nafasi ya kwanza. Youtube channel yako ikipata utazamaji mkubwa basi utapata kipato kikubwa sana. Kuna watu wengi wanategemea youtube channel kwa maisha yao. Wanalipa bill zao kupitia youtube.
Jinsi ya kufungua youtube channel
Ni rahisi sana. Unachotakiwa kuwa nacho ni gmail account. Kama hauna gmail account unaweza fungua kirahisi sana kwa kutembelea tovuti ya gmail account
Baada ya kukamilisha kufungua gmail account inakuwa rahisi kwani tayari umemiliki youtube channel. Ukiwa ume sign in gmail account, fungua tab nyengine na uweke address ya youtube.com. vile bado upo kwa google account, ile youtube channel itafunguka na jina yako ya gmail account. Kuanzia hapo ni rahisi maana utapata nafasi ya kubadilisha jina channel yako na baada ya hapo utakuwa unamiliki youtube channel.
Jinsi ya kuweka video kwa youtube
Baada ya kuifungua channel yako ya youtube basi ku upload video ni rahisi. Tazama hii picha hapa chini ndio uweze kuelewa zaidi
Kumbuka unaweza kuweka video nyingi utakavyo na haijalishi urefu wake bora tu uwe kwa internet. Video zikiwa nyingi kwenye channel yako inasaidia channel kujulikana kwa haraka. Kumbuka pia watu wengi wakitazama video kwenye channel yako, umaarufu wa channel unapanda zaidi.
Jinsi ya kukuza youtube channel
Unapofungua youtube yako lazima uwekeze. Kumbuka watu hawana ufahamu na channel yako. Lazima utumie watu wako wa karibu link ili wakusaidie ku share ndio channel yako ikue. Kuna wengi hulipia googleads ndio channel izidi kujulikana. Pia mitandao kama Facebook inaweza kukusaidia ku market channel yako kwa marafiki walioko huko facebook.
Malipo ya youtube
Malipo ya youtube hutegemea mambo kadha.
- Nchi yako
- Wenye wanatazama wako nchi gani
- Idadi ya wanaotazama
- Mda wanaotazama na kukaa kwa channel yako
- Kiwango cha dollar ama euro katika nchi yako
Kabla unaeze kupata mapato kwenye channel yako ya youtube, lazima uwe umefikisha subscribers 1000 na pia mda ya waliozitazama video zako uwe dakika Elfu nne.
Kulingana na utafiti wetu, ukiwa na kama 100,000 views huenda ukapokea $100. Kama nilivyosema hapo awali nchi ya wanaozitazama video zako inachangia kabisa mapato yako. Ukipata watazamaji wengi wa nchi kama vile America na U.K basi utakuwa na mapato zaidi.
Soma hii pia : wasanii bongo freemason