InternationalMaisha

Kim Kardashian adai talaka yake, hamtaki tena Kanye West

Kim Kardashian adai talaka yake, hamtaki tena Kanye West

Kim kardashian ambaye ni mume wake kanye west ako katika harakati ya kumtaliki mumewe. Wawili Hawa wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka saba. Kim kardashian anayejulikana sana ulimwengu mzima ashajaza makaratasi ya talaka huku akidai uhusiano wake na Kanye west haufai tena kwani Kila siku wanapitia misukosuko kwenye mapenzi yao.

Utaratibu wa talaka ya wawili hawa ulianza jumamosi tarehe 20 February 2021. Kiongozi wa Los Angeles superior court amedhibitisha kuwa kweli wawili hawa wamefungua kesi kuhusu talaka yao kwani walijaza karatasi zao ijumaa tarehe 19.

Kim kardashian ambaye kwa sasa ana miaka 40 ni mmiliki wa kipindi Cha television almaarufu reality Tv show.

Mnamo tarehe 14 October kim kardashian na Kanye west walionekana Miami Beach, Fl wakila chakula chao Cha jioni huku mapambo ya kimahaba yakionekana. Kwa miezi kadhaa wawili hawa hawajukuwa wakiishi pamoja. Hii Ina maana utaratibu wa talaka yao ulianza kitambo ila imekuwa siri kwa wengi.

Kanye west ambaye ni bilionea aliwahi kuwania kiti Cha urais wa marekani ila hakushinda. Hakuvunjika moyo kwani alisema mwaka wa 2024 atawania kiti hicho tena.

Uhusiano wao ulianza utata wakati Kanye west aliposhikwa na ugonjwa wa mfadhaiko wa akili ama kwa kimombo bipolar disorder.

Wawili Hawa walioana nchini Italy, Renaissance fortress ndani ya florence mwaka wa 2014. Wako na watoto wanne; North, saint, Chicago na Psalm. Urafiki wao ulianzia mwaka wa 2012 na mtoto wao wa kwanza walipata mwaka wa 2013.

Kim kardashian alikuwa kwenye uhusiano tofauti hapo awali na mchezaji wa NBA Kris Humphries lakini waliachana siku 72 baada ya harusi. Mwaka wa 2000, kim kardashian ambaye mda huo alikuwa na miaka kumi na tisa aliolewa na mtayarishaji wa mziki Damon Thomas. Mwaka wa 2003 Damon Thomas alimtaliki kim kardashian.

Soma hii ( Nandy aeleza mengi kuhusu mpenzi wake Billnass)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *