Siasa

William Ruto na Raila Odinga wataungana 2020, Moses Kuria asema.

William Ruto na Raila Odinga wataungana 2020, Moses Kuria asema.

Mbunge wa Gatundu south moses kuria amesema ana uhakika kuwa Raila Odinga na william Ruto watafanya Kazi pamoja. Moses kuria amesema wawili hawa huenda wakashikana ili kufanikisha ndoto za kuongoza nchi ya Kenya.

Akiongea kwenye mahojiano, moses kuria amesema Wawili hawa wataungana hata kabla ya mwaka wa 2022. Moses kuria alikuwa yuwahojiwa na Gerald Bitok ambaye ni mkaribu wa naibu wa rais william Ruto.

Moses Kuria Mp Gatundu south

” Nilikuwa wa kwanza kubashiri kuwa kutakuwa na handshake Kati ya Raila Odinga na Uhuru kenyatta na ikafanyika kweli.. pia nikasema Raila atafanya Kazi na jubilee na sasa mwajionea. Kwa hivyo naomba muniamini kwamba Raila Odinga na william Ruto mwaka wa 2022 kabla ya uchaguzi.. kuna watu wataachwa kwa mataa….”

Kuria aliongeza kwamba, ili Raila Odinga aweze kutumiza ndoto zake za kuongoza nchi ya Kenya, lazima aungane na naibu wa rais william Ruto. Kumbuka william Ruto na Raila Odinga walikuwa na uhusiano mzuri sana wa kisiasa mwaka wa 2007 kabla ya kutengana. Kama unakumbuka “pentagon” basi utakuwa unafahamu muungano wao huku wenzao wakiwa Musalia mudavadi, kalonzo Musyoka, Najib Balala na marehemu Joe Nyagah

Soma hii pia ( utajiri wa Raila Odinga)

Soma hii pia ( utajiri wa william Ruto)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *