Mchipuko

Maisha yangu iko hatarini, Juliani asema

Msanii wa mziki wa kufoka ama ukipenda hip-hop Julius Owino a.k.a juliani ameandikisha ripoti kwenye kituo Cha polisi Cha kilimani kwa kuhofia kuwa maisha yake iko hatarini. Kulingana na juliani ni kwamba, amekuwa akipokea meseji kutoka kwa mtu asiyemjua akitishia maisha yake.

Boniface Mwangi ambaye ni Mpiganiaji haki ya kisiasa aliandika hayo kwenye ukurusa wake wa Twitter akisema kuwa maisha ya juliani yamo hatarini na anapokea vitisho kwa mtu asiyemfahamu kupitia simu ya rununu.

Boniface Mwangi Twitter

Inasemekana mwenye kutuma hizo meseji alimhimiza juliani kutoweka picha zake wakiwa na Lilian Ng’ang’a aliyekuwa mke wa gavana wa machakos, Alfred Mutua

“Alimwambia juliani aache kupost picha zenye wako na Lilian Ng’ang’a kwa mitandao la sivyo watamuua,…. Boniface Mwangi aliandika kwa page yake ya Twitter … “

Julian life in danger

Jarida la kenyans.co.ke lilijaribu kumpigia juliani ili kupata ripoti kamili. Juliani alikubali kuwa asharekodi hiyo ripoti siku ya jumatano jioni katika kituo Cha polisi Ila hakutaka kuongea zaidi kuhusiana na hilo swala.

Tukio hili lilifanyika mda mfupi baada ya Lilian kutangaza kuachana na gavana wa machakos Alfred Mutua.

Alfred Mutua wife Juliani

“Katika maisha, lazima kuwe na mabadiliko na lazima tuheshimu hayo….. Kama miezi miwili iliyopita maisha yetu na Alfred Mutua yalichukua mwelekeo mpya na tukaja na maumizi ya kufikisha kikomo uhusiano wetu.. tulikuwa na maisha mazuri na ninashukuru mwenyezi Mungu kwa kutuleta sisi pamoja. Mimi na Alfred Mutua tutazidi kuwa marafiki…. Alisema Lilian”

Siku kadhaa zilizopita, Alfred Mutua aliandaa tamasha la kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake na akamualika aliyekuwa mkewe lilian nga’ng’a.

Soma hii pia: Harmonize afungua kituo Cha Radio na Tv

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *