Nasib jnr. Awakutanisha Tanasha na Diamond
- Nasib jnr. Awakutanisha Tanasha na Diamond
- Baada ya Zari Hassan kuwaleta watoto wake wamuone baba yao, Tanasha Donna naye amefuata nyayo
- Tanasha Donna na Diamond wali fanya tamasha pamoja.
- Video yaonyesha Tanasha na Diamond wakicheza pamoja.
- Diamond platnumz na mtoto wake Nasib jnr wanaonekana kuwa na wakati mzuri.
Kama utakuwa wewe ni mtu wa kufuatilia habari za burudani basi utakuwa ushakutana na hizi habari za Tanasha na Diamond Platnumz. Inaonekana Tanasha aliona hatowachwa nyuma na aliyekuwa mke wa Diamond, Zari Hassan.
Tanasha aliamua kumpeleka mtoto wake Nasib jnr kwa Babake. Safari hii nikama ilikuwa ya Siri maana wengi walifanya kukutana na picha za Nasib jnr na Babake diamond kwenye mitandao.
Baadae wawili hawa, Tanasha na Diamond walionekana kwenye tamasha usiku huo wakipiga show pamoja.
Haikujulikanawazi kama ilikuwa imepangiwa ama ilifanya kutokea tu. Kumbuka toka wawili Hawa waachane, Diamond hajapata nafasi ya kukutana na mwanawe.
Tanasha Donna na Diamond wanaonekana kuwa na ukaribu hata kama wawili Hawa waliachana. Sijui kama ukaribu wao ni wa mapenzi ama kinachowaleta pamoja ni mtoto wao Nasib jnr.

Baadae diamond yakuwachwa nyuma, ali post picha yake akiwa mdogo huku pembeni akimueka mtoto wake nasib jnr. Wawili Hawa waonekana kufanana na bila shaka hakuna DNA inayohitajika kubaini kama mtoto ni wake.

Tanasha Donna ni Kati ya wale wanawake wanaopendwa na mama dangote ambaye ni mamake Diamond. Kulingana na utafiti wetu, mama dangote anampenda sana Zari Hassan, mamake tiffa dangote. Wapili kwenye orodha hiyo ni Tanasha Donna ila anayeonekana kuchukiwa na mama dangote ni hamisa Mobetto.

Kwa sasa Tanasha Donna amekita kambi bongo huku habari za hapa na pale zikisema kwamba msanii huyu anatayarisha video yake mpya. Zidi kutegea habari zetu hapa mwangaza kwa habari za kuaminika.
Soma hii pia ( tazama wanawake warembo Tanzania)