Nyota ya Nadia Mukami yanazidi kung’aa
Nyota ya Nadia Mukami yanazidi kung’aa
Nadia Mukami ni msanii anayekuja kwa Kasi sana. Katika wale wasanii wapya ama ukipenda, wanaochipuka, Nadia Mukami atakuwa kwenye kumi bora. Mziki wake kwa sasa hivi unapendwa sana na watu wengi na huenda akawa msanii mkubwa na wakutegemewa duniani hivi karibuni.
Nadia Mukami ashapata tuzo kadhaa na mziki wake unawapa motisha vijana. Kusema kweli mziki wake upo tofauti. Kama unaipenda lugha ya kiswahili basi utakubaliana na Mimi kuwa maandishi ya huyu msanii ni ya Hali ya juu kwani anayajua sana mashairi.
Naweza nikasema talanta yake ni ya kipekee na pia ya kuzaliwa nayo. Kwa Sasa wengi wanajiuliza maswali, huyu Nandy anaweza kuwa ana date nani ama mchumba wake ni nani? Ama je, msanii huyu ana bwana?
Nadia Mukami ni msanii ambaye hapendi kuweka mambo yake hadharani ila yeye alifunguka na kusema ako naye mchumba. Kulingana na sababu zake mwenyewe, nadia Mukami alisema kuwa kwa sasa mchumba wake atazidi kumficha mpaka ile siku wawili Hawa wataona.
”… Nina boyfriend. Details are not important. Ile siku niko married ndio nitawaonyesha. Siezi enda kwingine. Yaani nilishamwambia by fire by thunder, we are getting married. You are not wasting my time. Lazima anioe…”
Nadia anaamini kwamba akiweka mahusiano yake wazi, wengi watajitokeza kumharibia uhusiano wao.
Hivi majuzi aliteuliwa kama mmoja wa kuwania tuzo za MTV Mama Awards. Hatua hiyo imezidi kumpa umaarufu zaidi na wasanii wengi kutoka nchi mbalimbali wanampigia simu huku wakitaka kufanya naye kolabo.
Nadia Mukami ft. Otile brown | Kolo
Nyimbo yake Kolo aliyoshirikisha Otile Brown inaendelea kupata utamazaji zaidi afrika kwa jumla na pia ipo ndani ya topten katika radio nyingi hapa afrika.
Soma hii pia ( Lavalava afunguka mazito anayoyapitia ndani ya wasafi label)