SiasaMchipuko

Raila Odinga; Uhuru Kenyatta wapo imara

Baada ya tetesi kuwa huenda kinara wa ODM Raila Odinga Kuungana na william Ruto, leo imejitokeza wazi kwamba Raila Odinga; Uhuru Kenyatta wapo imara.

Leo tarehe 31 March 2021, kiongozi wa O.D.M ( Orange democratic movement) bwana Raila Odinga amekutana na wanachama wake kuongelea kuhusu maendeleo na mambo yanayoendelea nchini kenya.

ODM party members

Yaliyozungumziwa kwenye mkutano huo ni pamoja na chanjo ya covid-19 na njia mwafaka za Kuzuia usambazaji wa virusi vya corona. Pia waliongelea kuhusu uchumi wa nchi kwa sasa na athari zake kwa wanainchi.

Waliohudhuria ni pamoja na Senata wa Minority Leader Hon James Orengo, chairman wa ODM Hon John Mbadi, National Assembly Minority Whip Hon Junet Mohammed, Secretary General Edwin Sifuna, Treasurer Hon Timothy Bosire na Hon Gladys Wanga.

Owner of ODM party

Raila Odinga amesema chama Cha odm kinaunga mkono muungano wake na Uhuru kenyatta almaarufu kama ‘handshake’ huku akimpongeza rais Uhuru kenyatta kwa kuleta uwiano na umoja Kati ya wakenya. Hii imesaidia sana kuweza kukagua mambo yanayoirudisha nchi nyuma na kutafuta mbinu mpya za kuweza kuleta maendeleo kwa nchi na wanainchi kwa jumla.

Raila Odinga aliwaomba wafuasi na wanachama wa O.D.M wazidi kuunga mkono handshake kwani Ina malengo makubwa ya hapa nchini na ulimwengu pia. Kingine kilichoongelewa pale ni BBI ambapo Raila Odinga alihakikishia wanainchi kuwa wanachama wa ODM wanaunga mkono BBI ( Building bridges intiative) na katiba.

Raila Odinga aliwaomba wabunge kuweza kushughulikia BBI ili waweze kuiachia wanainchi ndio wanainchi waweze kutoa maamuzi yao kuhusu BBI. Baada ya hapo kuibadili katiba itakuwa rahisi.

Bali na BBI, Raila Odinga amewaomba wanainchi wazidi kuzingatia afya zao wakati huu wa corona na wafuate sheria zinazotolewa na wizara ya afya. Aidha alitaka wanainchi waweze kupata chanjo ya covid-19 ili nchi na ulimwengu kwa jumla waweze kupigana na kushinda vita dhidi ya ugonjwa huu

Aliomba serikali iweze kuja na mbinu mpya za kuwezesha wanainchi kuishi na hii hali gumu ya maisha wakati huu wa lockdown.

Soma hii pia ( utajiri wa william Ruto)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *