Mchipuko

Shaffie Weru Homeboyz radio na wenzake wawili wamesimamishwa Kazi.

Shaffie Weru Homeboyz radio na wenzake wawili wamesimamishwa Kazi. Watatu hawa walikuwa wanafanya Kazi Homeboyz radio.

Tukio hili likitokea ijumaa baada ya matamko yao mabaya kuhusiana na mwanamke aliyerushwa kutoka gorofani na mwanaume wake baada ya kumkatalia tendo la ngono.

Wenzake wawili waliosimamishwa Kazi ni pamoja na Dj Joe Mfalme na mtangazaji mwenzao kwa jina Naville. Watatu hawa hufanya kipindi kwa jina “Left Off” kinachopeperushwa asubuhi.

Mwanamke aliyerushwa kwa gorofa Anajulikana kama Eunice Wangari Wakimbi mwenye umri wa miaka 20. Alirushwa kutoka gorofa ya kumi na mbili hadi chini na mwanaume waliyekutana naye facebook. Tukio hili lilifanyika tarehe 12 March 2021.

Homeboyz walitangaza kuwasimamisha Kazi watatu Hawa kwa wiki mbili kama kuwapa adabu.
Meneja wa Homeboyz radio bwana Somoina Kimanjino alisema watangazaji wa radio ya Homeboyz watapelekwa masomo ya lazima kuhusiana na chenye wanafaa kuongea na kutangaza hewani na chenye hawafai. Hii ni pamoja na mambo yanahusiana na jinsia tofauti kama vile vita vya kijamii na mambo mengi haswa yanayohusu wanawake.

Video ya akina shaffie Weru Homeboyz na wenzake ilikuwa kuhusiana na walichokisema kuwa wanawake wanafaa kuwa wagumu kwa Wanaume na wasiwakubalie haraka. Aidha waliwalaumu wanawake kwa kukubali kuwafanyia wanaume kila kitu hata kwenda kulewa nao. Mwenye alikuwa anashikika akiongea sana ni shaffie Weru huku mtangazaji mwenzake Naville akisikika akicheka.

Shaffie na Dj Joe waliomba msamaha kutokana na maneno yao yaliyowakwaza wanawake na wakenya wengi kwa jumla

“Nachukua fursa hii kumuomba msamaha kwa kuongea maneno yanayoonekana kuchangia Vita dhidi ya wanawake. Nimejuta sana kwa maneno yangu kwani nimeongeza machungu kwa vita ambavyo vyanavyoendelea tayari. Sitaki kuwa mmoja wa kuchangia Vita dhidi ya wanawake na kuanzia sasa nitachangia kumaliza vita dhidi ya wanawake pamoja na watoto… Alisema shaffie Weru.

Hii sio Mara ya kwanza Homeboyz radio kuomba msamaha. Mwaka wa 2019, Homeboyz radio ilisimamisha show moja pamoja na Didge ambaye alikuwa mwendeshaji wa kipindi hicho. Hii ni baada ya Didge kumkejeli Ivy Wangechi mwanafunzi wa somo la dawa ama kwa kimombo “medical student”. Didge alitamka maneno yaliyoonekana kumkejeli Ivy Wangechi huku watangazaji wenzake wakionekana kufurahia maongezi hayo. Didge alisikika akiwashauri wanawake wafanye uchaguzi wa busara kwa wanaume waonaowataka kuolewa nao kwani wanaweza kuwa wanachagua njia ya kifa chao

Ivy Wangechi aliuwawa ndani ya Moi Referral hospital in Eldoret alimokuwa anafanya mtihani wake wa mwisho. Mshukiwa mkuu Naftali Njahi alisemekana kumpiga Ivy Wangechi na shoka kabla ya kumchinja.

Soma hii pia ( maisha na masomo ya rais wa tanzania Suluhu Hassan)

Didge baadaye aliomba msamaha kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa mafans wake wote aliowakwazwa.

Tazama video 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *