MaishaMchipuko

Top 10 ya matajiri Tanzania 2020

Top 10 ya matajiri Tanzania 2020  iliotolewa hivi majuzi inaonekana kubadilika kiasi na sio Kama ya mwaka Jana. Kuna watanzania zaidi tofauti wameingia kwenye hiyo orodha.

Tanzania inajulikana kuwa na matajiri wengi Ila wengi huwa hawapendi kujiweka wazi. Labda hawapendi maisha ya kujionyesha ama pia wanaogopa kuvamiwa na wahalifu.

Ifuatayo Ni orodha inayojumuisha Top 10 ya matajiri Tanzania 2020

1. SAID BAKHRESA

tajiri said bakhresa

Jina lake kamili ni Said Salim Awadh
Bakhresa. Jarida la Forbes mwaka jana,
lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri
40 Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye
thamani ya dola milioni 620 (karibu
shilingi trilioni moja). Hata hivyo,
inadaiwakuwa tabia ya usiri wa Bakhresa
inafanya mali zake zisijulikane sana, ila ni
tajiri zaidi ya kiwango hicho.Ndiye
mmiliki wa makampuni ya Bakhresa
yanayotoa bidhaa zenye chapa ya Azam
ambazo zinauzwa nchi mbalimbali Afrika.
Ana viwanda vya nafaka na vinywaji,
vyombo vya usafiri wamajini, uuzaji wa
chakula, bidhaa za plastiki na kadhalika.
Ndiye mmiliki wa Klabu ya Azam FC.

2. GULAM DEWJI

Gulam dewji
Huyu ni baba wa mfanyabiashara
maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’.
Jarida la Forbes mwaka jana lilimtaja
kuwa na utajiri wenye thamani ya dola
milioni 560 (karibu shilingi bilioni 900).
Mafanikio yake kibiashara yalianza
mwaka 1970. Kiwanda chake cha 21st
Century Textiles, kinatajwa kuwa moja ya
viwanda vikubwa vya nguo Afrika.

3. ROSTAM AZIZ

Rostam Azizi
Inadaiwa anamiliki utajiri wenye thamani
ya dola milioni 420 (shilingi bilioni 672).
Anamiliki karibu asilimia 40 ya hisa
Kampuni ya Vodacom Tanzania. Ni
mmiliki wa Kampuni ya Caspian
inayohusika na uchimbaji wa madini na
ukandarasi nchini Tanzania, nchi kadhaa
za Afrika na Asia.

4. DK. REGINALD MENGI

Dr. reginald mengi
Anatajwa kumiliki utajiri wenye thamani
ya dola milioni 280 (karibu shilingi bilioni
450). Ni mmiliki wa kundi la makampuni
ya IPP, yanayomiliki vyombo vya habari,
viwanda, migodi ya dhahabu, Tanzanite
na kadhalika.

5. ALI MUFURUKI

Ali mufuruki
Utajiri wake unatajwa kuwa na thamani
ya dola milioni 110 (shilingi bilioni 176).
Nimmiliki wa kundi la makumpuni ya
Infortech Investment, inayomiliki maduka
yanayouza vitu vya rejareja Tanzania na
Uganda. Vilevile ana vitega uchumi
vingine.

6. MUSTAFA SABODO

mustafa sabodo
Ni mfayabiashara mkubwa sana nchini
anayemwaga mamilioni kwa misaada.
Wakati wa kuanzishwa kwake, aliipa
Taasisi ya Mwalimu Nyerere shilingi
milioni 800, akasaidia shilingi milioni 100
katika mradi wa kustawisha mimea jamii
ya kunde. Vilevile alikipa Chadema
shilingimilioni 300. Inadaiwa kuwa utajiri
wake unazidi shilingi bilioni 100.
Kampuni yake ya Khoja Shia Itnasheri
Jamat (KSIJ), ndiyo yeye tenda ya kujenga
maeneo ya maegesho ya magari Posta, Dar
es Salaam, mradi wenye thamani ya
shilingi bilioni 5.6.

7. ABDUL-AZIZ ABOOD

Abdul Aziz Abood
Kiwango chake cha utajiri hakiwekwi sana
wazi lakini anatajwa kuwa miongoni mwa
mabilionea 10 wanaotikisa nchi kwa sasa.
Anamiliki viwanda kadhaa mkoani
Morogoro, vyombo vya habari, Abood
Radio na TV. Anamiliki mabasi ambayo
yanafanya safari zake kati ya Morogoro,
Mbeya na Dar es Salaam. Ni Mbunge wa
Morogoro Mjini (CCM).

8. MICHAEL SHIRIMA

michael shirima
Ni mmiliki mkuu wa Shirika la Ndege la
Precision ambalo linafaya safari zake
ndani ya Tanzania pamoja na nchi
mbalimbali za Afrika. Ana asilimia tano
yahisa katika Beki ya I&M (Tanzania),
vilevile ni memba katika bodi ya
wakurugenzi wa benki hiyo yenye
thamani ta shilingi bilioni 200. Hisa zake
Precision ni asilimia 42.91.

9. YUSUF MANJI

yusuf manji
Kiwango halisi cha utajiri wake bado
hakifahamiki lakini anafahamika kama
mmoja wa mabilionea wakubwa nchini
Tanzania. Ni mmiliki wa makampuni ya
Quality Group na majengo ya Quality
Centre, Quality Plaza na kadhalika. Ni
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na utajiri
wake umeifaya timu kutotetereka tangu
alipoanza kuiongoza.
Insurance

10. MOHAMMED DEWJI

mohammed dewji

Baba yake anashika nafasi ya pili katika
orodha hii. Dewji au Mo kama
anavyoitwana wengi, anatajwa kuwa
bilionea nambari moja katika orodha ya
mabilionea vijana Afrika (orodha hiyo
tuliitoa wiki iliyopita). Ni mmiliki wa
makampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Limited (METL) ambayo
inatengeneza faida ya shilingi bilioni 136
kwa mwaka

Hao ndio Top 10 ya matajiri Tanzania 2020. Endelea kufuatilia mwangaza news kwa Habari Moto Moto

Soma hii pia ( wasanii matajiri duniani)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *