HistoriaMaisha

Ugomvi wa Willy Paul na Diana bahati

Ugomvi wa Willy Paul na Diana bahati ndio habari ya mjini na kama basi hujapatana na hii habari basi utakuwa umepitwa sana ila usiwe na wasiwasi kwani hapa mwangaza news tumeandaa kama ilivyotendeka.

Kama umekuwa ukifuatilia mitandao Kuna mambo yanayoendelea Kati ya Diana bahati na Willy Paul. Wawili hawa wamekuwa wakigonga vichwa vya habari baada ya Diana bahati kurekodi video akielezea kuwa Willy aliwahi kumshika kwa nguvu.

Hivi majuzi, Diana Marua alirekodi video akielezea mengi kuhusu Willy Paul. Kulingana na Diana, willy Paul aliwahi kujaribu kumnajisi. Hii ni kabla ya bahati na Diana kuoana. Diana alieleza kuwa Kuna wakati yeye na Willy Paul walikuwa kwa tamasha na willy Paul akaomba kutoka na Diana Marua mpaka nyumbani kwake ili wakafanye mazungumuzo mhimu.

Diana bahati alikataa wito wa Willy Paul na kumwambia kama Kuna chochote angependa kuongea naye waweza kuongea hapo ndani ya tamasha kwani hangeweza kwenda naye kwake nyumbani juu walikuwa hawana mazoea.

Willy Paul alimueleza Diana Marua kwamba Jambo lenyewe lilikuwa la faraga na hangeweza kumtamkia sehemu ya watu wengi hivo basi akamuomba Diana Marua aje waongee ndani ya gari yake. Diana Marua alimkubalia na akaingia ndani ya gari ya Willy Paul.

Alipoingia kwa gari willy Paul alianza kuendesha gari huku akiwa ameweka Loki kwa milango yote. Kulingana na Diana, willy Paul aliendesha gari mwendo wa Kasi sana na Diana hangeweza kumsumbua Willy Paul kwani alihofia kupata ajali.

Walienda moja kwa moja mpaka sehemu Willy Paul alikuwa akiishi. Wakiwa kwenye gari. Willy Paul alikuwa akimshikashika kimapenzi Diana Marua japo Diana alikuwa akimuomba Willy Paul kuachana naye.

Ndani kwa Willy Paul, Diana Marua alishikwa kilazima na willy Paul ila kwa bahati nzuri Diana Marua aliweza kujitoa kwa mtego wa Willy Paul. Japo nguo zake Diana zilikuwa zimeraruriwa, aliweza kutoroka kupitia bodaboda.

Baada ya video hiyo ya Diana bahati kuwekwa kwa YouTube, willy Paul alijitetea na kusema kwamba hakumlazimisha Diana Marua kufanya mapenzi na yeye. Kulingana na willy Paul, wawili hawa wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya Diana kukutana na Bahati.

Kwa sasa ni vigumu sana kujua anayeongea ukweli Kati ya hawa wawili. Mpaka sasa, bahati ambaye ndiye mume halisi wa Diana Marua bado hajaongea chochote Kulingana na hilo tukio. Hapa mwangaza news nasi tupo masikio na macho wazi tukitegea mengi kuhusiana na Ugomvi wa Willy Paul na Diana bahati.

Tegea hapa mwangaza news kwa mengi zaidi na chochote kile kitakachotokea kuhusiana na habari hizi za Diana na willy Paul, basi wewe utakuwa wa kwanza kufahamu hiyo taarifa.

Pia Soma : vita Kati ya bahati na Willy Paul

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *