MzikiSanaaYoutube videos

Video ya anjella – Nobody yafikisha views million YouTube kwa mda wa siku moja

Kama basi utakuwa hujaipata, habari ni kwamba Video ya anjella – Nobody yafikisha views million YouTube kwa mda wa siku moja. Ni juzi tu video ya harmonize na Awilo Longomba ilifikisha million mbili kabla ya masaa ishirini na nne.

Je, ni mbinu gani kampuni hii ya konde Gang yatumia kufukisha views nyingi kwa siku kidogo?. Wengi wamekuwa wakitaka kujua kama msanii harmonize ananua views au la. Kulingana na gwiji mmoja wa mambo inayohusiana na google inayomiliki YouTube, ni hatia kununua views hata kama kunazo kampuni za kuuza views.

Video ya anjella - Nobody yafikisha views million YouTube kwa mda wa siku moja

Kulingana na gwiji huyu wa tekinologia, huenda ukapata faini kama utazoea kununua views na hata unaweza kupoteza chaneli yako ya youtube.

Jambo la kwanza YouTube wanalolifanya wakikupata na hatia ya kununua views, huwa wanasimamisha matangazo almaarufu kama google adsense zinazowapa Wana YouTube pesa. Kunayo njia moja tu youtube wanaruhusu ili uweze kukuza youtube channel ama views zako, nayo ni kutumia matangazo ya google ads. Njia hii sio mojawapo ya kununua views Ila Ina tangaza video yako ndio iweze kuwafikia wengi watazamaji.

Nachojaribu kusema ni kwamba kama account ya YouTube ya harmonize  bado ipo na haijafutwa na kampuni ya google, basi msanii huyu anatumia njia sahihi ya kupata views. Na pia ukitazama vizuri kwenye video zake zilizoko YouTube, utakutana na ads. Hii Ina maana Harmonize hajakiuka sheria yoyote kutoka kwa kampuni ya youtube.

Kama – Anjella na harmonize

Kwa wale walidhania labda msanii huyu ananua views basi sio kweli ila anachokifanya ni kutumia matangazo kwa njia ya google ads inayokubalika na kampuni ya google.

Kwa Mara ya kwanza tazama video ya nobody – anjella

 

 

 

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *