Zeddy comedian ni mwanamke ambaye kazi yake ni ya uchekeshaji ndani ya Churchill show. Ameonekana kukerwa na yanayofanyika pale Churchill na inaonekana kuna mengi sana yamefichwa.
Churchill
Zeddy comedian hakuanza Leo ila inaonekana alianza kukerwa na uongozi wa Churchill wakati wa kifo Cha njenga mswahili ambaye pia alikuwa mchekeshaji pale Churchill show.
professor Hamo Churchill show
Kulingana na yeye, director wa Churchill show anachangia wasanii wa Churchill kupoteza mwelekeo wao wa maisha kwa dhulma wanazowafanyia. Kwa sasa wasanii watatu wameaga dunia kutokana unyogovu ama depression kwa kimombo.
Chenye kinamshangaza zeddy, Churchill haifanyi juhudi zozote ili kuwasaidia wasanii hawa chipukizi. Hii ndio sababu zeddy aliamua kuweka wazi kwa mtandao ili kuonyesha wanainchi kinachotendeka Churchill show
Mazishi ya Njenga mswahili
Wakati Njenga mswahili alipoaga dunia, zeddy comedian aliweza ku post kwenye Facebook na akawaomba wananchi wawe wakiwaeka karibu wasanii kwani wanapitia hali ngumu. Wakati huo huo aliongelea kuhusu kasee aweze kusaidiwa Wala sivyo angepatwa na msiba. Kwa sasa kauli yake imetimia kwani kasee hayuko Tena duniani ashaaga dunia
Kulingana na zeddy comedian, wasanii watatu wa Churchill; Njenga mswahili, Ayieya poa na Kasee wameaga dunia baada kupoteza nafasi zao za kazi ndani ya Churchill Show.
Hivi ndivyo alivyoandika kwenye Facebook yake,
Long post alert!
Ndio huyu mzizi wa fitna @VictorBer24 creative director wa Churchill Show “Depression maker”. Kama ushaiwai enda auditions za Churchill show, hakika unajua huyu msee.huwa hearltess, roho chafu kuliko ya Firaun (farao) yaani atakuthalilisha na maneno yake makali kuliko moto wa jehanam (hell) Atafanya ujidharau maisha yako yote! Kwa wale hawajui, ndio perform Churchill lazima uende rehearsal 3days so Ber hatakwambia day one hajafeel jokes zako.Atakufanyisha P.E hadi siku ya kurecord show,kama bado 2hrs anatoa program ya wale wata perform.Ukiangalia list ya performers unapata jina lako haliko. Ngai hapa ndo unaonga msanii ameanza kupata stress coz umekam three days umetumia fare, ukabuy nguo ya kuchapa show ama ata ukakopa,unapata msanii amefanyiwa hivi like three months.Imagine, wewe kama msanii, bado unarudi juu comedy ni inborn; unaskianga tu kuperform. Ukipata bahati upenye alafu uanze kushine, Ber anaanza kukuua pole pole; utaenda rehearsal ataskiza kila mtu kama umekaa hapo amke na aende bila ata kukuambia lolote, unabaki na viulizo. Unaeza enda rehearsal akuite akuulize leo ni when, ukimjibu anakwambia ukam next year siku kama ya leo na hujamkosea ata!
YY comedian Churchill show
Aliendelea kueleza vile ashawahi kumbembeleza Victor Ber nafasi ya ku perform. Alisema director huyu huwa na kiburi maana yeye ndiye huchagua wasanii watakao panda kwa jukwaa.
Victor Ber
Kulingana na zeddy comedian, Victor Ber amechangia pakubwa sana kuwaharibia wasanii maisha yao. Hii ndio sababu iliyomfanya aweke wazi.
Aliendelea na kusema;
Anaeza pata umeandikwa kwa program tayari umepakwa makeup na akutoe bila sababu,yaani Ber hua ameweka wasanii na baridi utadhani tuko(Netherlands)anataka umuabudu laa si utakipata,wasanii hulamba huyu msee hadi kale kachumvii ka? si eti mimi ni shujaa zii ni vile nimekaa makaburi miaka 5 nikajua hii dunia si mama ya mtu; story for another day reason naandika hii ndio upcoming wale wanakam wasipitie yale tumepitia Ber, Njenga alikulilia hadi siku ya mwisho ndio mauti yamfikie? Alikol mara ngapi?After nimepost natafuta Kasee mlimtafuta mkampumbaza siku chache ukamchocha atakua anachapa show alikuja rehearsals mara mingi sana lakini wapi ukamwambia ataperfom show ya Machakos. Kufika huko ukamyima show. Swali ni,je, utaumiza wasanii hadi lini? Wasanii waitaishi na Depression hadi lini. Pliz Comedians msicomment hamtawai pewa show mimi nishachoma,lakini, ile siku mtajua Mungu ndiye hupeana riziki hamtawahi lamba mtu makwapa.