InternationalMchipuko

Nchi tajiri duniani

Nchi tajiri duniani; Ushawahi kujiuliza kwa nini pombe huuzwa ghali mahali kwingine na ikauzwa karibu na bure sehemu nyingine ya ulimwengu? Sababu mojawapo ni bei ya ubadilishaji fedha za kitaifa lakini sababu kubwa ni kuwa sehemu zingine ni tajiri kuliko zingine kama maonyesho yetu ya hivi karibuni yalivyoashiria

Nchi tajiri zaidi Ulimwenguni

Kuna nchi nne duniani zenye pato la nchi kwa mda maalum la zaidi ya dola elfu mia moja:

  • Qatar ($138.9k)
  • Macao ($113.4K),
  • Luxembourg ($112K)
  • Singapore ($105.7K)

Nchi tajiri zaidi duniani huwa na idadi ndogo ya watu. Kwa mfano bara Asia, China, India na Japani haziko katika bora kumi

Marekani hata haipo karibu kuwa nchi tajiri zaidi kwa kiwango cha pato la nchi kwa mda maalum. Hata ingawa ya juu zaidi Marekani ni $67.4K, Marekani iko katika kiwango cha kati ulimwengu mzima

Afrika ni maskini zaidi. Nchi mbili tajiri zaidi hata haziko kwenye ramani, Ushelisheli ($33.1K) na Mauritius ($26.5K)

Tulipata takwimu zetu kutoka kwa Benki kuu ya Ulimwengu ya 2020. Kiwango cha pato kwa mda maalum huwa inapima uchumi wa nchi ikilinganishwa na idadi ya watu katika nchi hiyo. Hii idadi ni muhimu kwa sababu nchi zenye idadi kubwa zaidi ya watu kama China ama India inaweza kuinua kiwango cha pato kwa mda la nchi na bado kuwe na mamilioni ya walala hoi. Benki kuu ya ulimwengu husawazisha takwimu zake ili ipate uwezo wa ununuzi ambao huwezesha ubadilishanaji wa fedha za kigeni.

Tumetumia rangi maalum katika bendera ya kila nchi ili kuonyesha wanaojiweza na wasiojiweza.

Nchi kumi tajiri zaidi ulimwenguni – Kiwango cha pato kwa mda maalum (2020)

  1. Qatar: $138.9K
  2. Macao: $113.4K
  3. Luxembourg: $112K
  4. Singapore: $105.7K
  5. Ireland: $87K
  6. Brunei Darussalam: $85K
  7. Norway: $79.6K
  8. UAE: $70.4K
  9. Kuwait: $67.9K
  10. Switzerland: $67.6K

Nchi zenye kiwango kikubwa cha pato kwa mda maalum husawazisha uwezo wa ununuzi huwa ni majimbo madogo ambayo ni tajika ulimwenguni katika viwanda maalum. Nchi tajiri zaidi ulimwenguni, Qatart ($138.9K) ni nchi ndogo Mashariki ya kati yenye matimbo ya mafuta. Macao ($113.4K) ni nchi ndogo ambapo watu matajiri kutoka Asia huenda kucheza kamari. Hizo nchi zingine mbili kufikia $100K ni nchi ndogo vile vile Luxembourg ($113K) na Singapore ($105.7K)

Marekani haipo kwenye orodha ya nchi 10 tajiri zaidi. Amini usiamini Marekani ndio nchi tajika zaidi ulimwenguni lakini sio nchi tajiri ukikusudia kiwango cha pato kwa mda maalum. Marekani iko katika nambari 12 na $67.4K ikiwa nyuma ya Switzerland ($67.6K) na Kuwait ( $67.9K). Kwa kusudia haya Marekani ndo nchi Tajiri zaidi Marekani zaidi ya Canada ($52.1K). Sehemu iliobakia iko katika kiwango chini ya $50K

Mtazamo wa mwisho kutoka kwenye maonyesho yetu ni kuwa Afrika ndo sehemu maskini kabisa ikilinganishwa na sehemu zingine za ulimwengu. Imewekwa katika nafasi ya karibu na kifo katika kipimo chochote cha utajiri na viwango vya maisha, hamna nchi hata moja ya Afrika iliyo na kiwango cha pato kwa mda maalum cha $50K na zaidi. Nchi mbili za juu zaidi Afrika ni Ushelisheli ($33.1K) na Mauritius ($26.5K) ambazo hazipo katika ramani yenyewe. Asilimia kubwa ya Afrika ipo katika kiwango cha pato kwa mda cha chini ya $10K ambayo ni kiwango cha chini zaidi katiko nchi zilizoimarika kiuchumi ulimwenguni

Soma hii pia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *