Youtube videosMaishaMziki

Mkubwa Fella: Sihusiki kabisa na kushuka kwa Aslay

Mkubwa Fella ama ukipenda mkubwa na wanawe ameeleza kwamba yeye hahusiki kabisa na Kushuka kwake Aslay. Ni mda sasa Aslay hajakuwa akigonga vyombo vya habari. Ni Miezi mingi imepita kabla msanii huyu kuachia hit song. Wengi wamekuwa wakijiuliza tatizo ni nini huku wengi wakilaumu Wasafi media kwa kupotea kwa Aslay kwenye game la Mziki.

Mkubwa fella Diamond

Katika mahajiano na Mkubwa Fella na Mbengo Tv nchini Tanzania, Fella alisema anasikita na jambo hilo. Alisema yeye anaamini kwamba Aslay anajipanga vizuri na hivi karibuni huenda akafanya maajabu ila akaongeza kwamba, itakuwa jambo la kusikitisha kama Aslay atakuwa amelemewa na Mziki. Mkubwa Fella alieleza kwamba yeye aliachana na Kikundi cha yamoto band na kwa sasa ako na Mbosso peke yake kwenye label ya wasafi. Mkubwa Fella ni Mmoja wa meneja katika wasafi media hii ina maana anahusika na mipangilio ya Mbosso ambaye amesajiriwa kwenye label ya wasafi media.

Mkubwa Fella alipoulizwa kilichowafanya yamoto band kuvunjika, alisema hana uhakika ila kuna uwezekano waliona hawapati kila kitu kwake hivyo basi wakaamua kwenda kutafuta zaidi huko nje. Hivi sasa mkubwa Fella ni mbunge na anatumikia wakati wake mwingi kuwafanyia kazi wanainchi waliomchagua. Kumbuka Mkubwa Fella ndiye alikuwa mwanzilishi wa Yamoto band na wakati huo alikuwa akifahamika zaidi kama mkubwa na wanawe. Kuna wasanii wengi walijulikana kupitia mkubwa na wanawe wakiwemo Chege na Temba.

Chege temba mp3 downloads

hapo awali baada ya kikundi cha Yamoto kuvunjika, Aslay alijitahidi sana na kuonesha uwezo mkubwa wa kikazi bila uwekezaji wa meneja yeyote. Wengi walimsifia na hata kuona kama alikuwa akipoteza mda wakati alipokuwa Yamato band. Nyimbo zake zilipata umaarufu Mkubwa dunia nzima na aliweza kufanya tamasha nyingi sana Tanzania na sehemu mbalimbali ulimwengu mzima.

Sio Aslay peke yake ambaye ako chini kimuziki kwa sasa. Wapo wasanii wengine kama vile Temba, Chege, na wengineo. Kumbuka wasanii hawa wote walikuwa tishio kwa soko la mziki wa bongo flava ila kwa sasa wamenyaza. Mziki wa Bongo una ushindani mkubwa sana na kila siku wasanii wapya wanachipuka. Ni hivi maajuzi Rayvanny alifanya utangulizi wa msanii mpya kwa jina Macvoice. Sio huyo tu kwani Harmonize naye ana wasanii karibia watano kwenye label yake. Hii ina maana soko la mziki wa bongo lipo na ushindani mkubwa sana na usipofanya bidii huenda ukabaki nyuma.

Aslay child Aslay songs 2021

Kwa mda sasa mambo yanaonekana kwenda mrama kwa msanii huyu na kila anapoachia nyimbo inakataa katakata kuwa kubwa kama hapo awali. Media za Tanzania nazo zinaonekana kama hazimpi sapoti na ni kama wameelezana. Hatujui tatizo linatokea wapi ila labda nyimbo anazozitoa Aslay hazijafika kiwango cha kuchezwa sana kenye vyombo vya burudani tofauti na hapo awali.

aslay mbosso

Nyimbo iliyoonyesha uwezo wa Aslay ni Angekuona(Mama) ambayo aliachia mda mfupi baada ya kifo cha mamake. Nyimbo hii ilipendwa zaidi japo wengi walifikiria haitakuwa kubwa kwani video yake ilikuwa ya kawaida. Nyimbo hii iliandikwa kwa makini sana na ukuiskiza utakujua Aslay alikuwa na hisia za ukweli wakati alikuwa akiandika nyimbo hii. Nyimbo zaidi zilifuatana ikiwemo kolabo yake na nandy Subalkheri Mpenzi iliyopendwa zaidi. Sio hizo tu, Aslay ana nyimbo zaidi Nzuri ambazo mpaka sasa zinachezwa sehemu nyingi za ulimwengu.

ieleweke kwamba, Maisha huwa ina kupanda na kushuka na ni lazima tukubali kwamba kila kitu kipo na wakati wake. Msanii akishuka huwa vigumu sana kupanda ila hii haimanishi msanii hawezi akapanda tena. Kuna wengi washapotea na wakarudi kwenye game kama wasanii wapya. Unachotakiwa kufanya ni kuwa na bidii na kuangalia ni wapi ulikosea na baada ya hayo yote unafanya marekebisho na kuanza tena upya.

Hapa Mwangaza news tunamuombea msanii huyu aweze kurudi Kwenye game kwani tunaitamani sauti yake na mashairi mazuri. Asanteni sana kwa wale wamekuwa wakifuatilia taarifa za hapa mwangaza news. muendelee na Moyo huohuo.

Soma hii pia: Maisha ya mbosso baada ya yamoto band kuvunjika

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *